Rais wa Romania Klaus Iohannia, na katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg wametoa wito kwa muungano wa NATO kuimarisha msaada wake kwa Ukraine, na kuonya kwamba kuna hatari kubwa ya kiusalama eneo hilo, ambayo haijawahi kuonekana.
Rais Iohannia amesema kwamba muungano wa NATO unaendelea kuimarisha shughuli zake katika eneo la Baltic na black sea kwa lengo kubwa la kuimarisha usalama.
Mkuu wa NATO amesema kwamba sehemu za mapambano zimeundwa, ikiwemo sehemu inayoongozwa na Ufaransa nchini Romania, huku ndege za kivita za Canada zikisaidia kuhakikisha kwamba anga ya nchi wanachama inasalia kuwa salama, huku makombora ya Marekani yakikihakikisha kwamba mfumo wa ulinzi wa NATO unasalia kuwa imara.
Stoltenberg amesema kwamba watachukua kila hatua kuhakikisha kwamba wanalinda nchi wanachama, akiongezea kwamba msaada unaendelea kutolewa kwa nchi zinazokabiliwa na tisho la usalama kama Bosnia Herzegovina, Georgia, na Moldova.
Ukraine imeomba sialaha zenye uwezo mkubwa
Waziri wa ulinzi wa Ukraine Dmytro Kuleba, ameambia mkutano mawaziri wa mambo ya nje wa nchi saba za Nordic na Baltic kwamba nchi yake inahitaji silaha zenye uwezo mkubwa wa kulinda anga yake ili kukabiliana vilivyo na mashambulizi ya makombora ya Russia yanayolenga mfumo wake wa nshati.
Kuleba alikuwa na maafisa wa serikali za Estonia, Finland, Iceland, Latvia, Lithuania, Norway na Sweden katika kikao cha jana jumatatu, kabla ya kuanza kwa kikao cha mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama cha NATO, leo jumanne na kesho jumatano.
Kuleba ameambia mawaziri kikao hicho kwamba silaha za kulinda anga zitawezesha Ukraine kulipua makombora ya Russia na kuzuia uharibifu dhidi ya mfumo wa nshati unaotokea kila mara.
Mawaziri hao wamekubaliana kuongeza msaada zaidi wa mfumo wa ulinzni wa anga ya Ukraine.
Waziri wa mambo ya nje wa Estonia Urmas Reinsalu ameambia shirika la habri la Reuters kwamba nchi za magharibi zinastahili kuhakikisha kwamba Ukraine inashinda vita dhidi ya Russia kwa kutoa msaada wa kutosha wa silaha, zikiwemo makombora ya masafa marefu.