Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 20, 2024 Local time: 05:40

Ukraine imetungua ndege 42 zisizo na rubani za Russia


Mfano wa Drone
Mfano wa Drone

Mapambano ya anga  yamekuja siku moja baada ya ndege isiyo na rubani ya Ukraine kupiga  ghala katika mkoa wa Tver nchini Russia.

Ukraine imesema leo Alhamisi kuwa kitengo chake cha ulinzi wa anga kilitungua ndege zote 42 zisizokuwa na rubani ambazo Russia ilizitumia katika mashambulizi ya usiku kucha ikilenga mikoa mbalimbali nchini humo. Jeshi la anga la Ukraine limesema pia lilitungua kombora lililoongozwa na Russia.

Mashambulizi ya ya drone za Russia yalielekezwa katika mikoa ya Cherkasy, Dnipropetrovsk, Kherson, Kirovohrad, Kyiv, Mykolaiv, Rivne, Vinnytsia, na Zhytomyr. Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema imeharibu ndege mbili zisizo na rubani za Ukraine katika mkoa wa Kursk, na Drone nyingine katika mkoa wa Belgorod.

Mapambano ya anga yamekuja siku moja baada ya ndege isiyo na rubani ya Ukraine kupiga ghala katika mkoa wa Tver nchini Russia, na kusababisha moto mkubwa na kuwalazimisha watu kuhamishwa katika eneo hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG