Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Agosti 13, 2024 Local time: 00:07

Ukraine imepiga Russia kwa kombora la masafa marefu


Wanajeshi wa Russia wakitekeleza mashambulizi dhidi ya Ukraine July 12 2024
Wanajeshi wa Russia wakitekeleza mashambulizi dhidi ya Ukraine July 12 2024

Bohari la kuhifadhi mafuta limewaka moto katika jimbo la Rostov kusini magharibi mwa Russia kufuatia shambulizi la ndege zisizokuwa na rubani za Ukraine mapema Jumamosi.

Maafisa wamesema kwamba shambulizi hilo la masafa marefu lililotekelezwa na wanajeshi wa Ukraine limetokea sehemu ya mpakani.

Ukraine imeimarisha mashambulizi ya angani dhidi ya Russia katika miezi ya hivi karibuni, ikilenga viwanda vya kusafisha na kusambaza mafuta katika juhudi za kupunguza mashambulizi ya Russia.

Jeshi la Moscow linaendelea kufanya mashambulizi mashariki mwa Ukraine, ambako wanajeshi wa Ukraine wanakabiliwa na uhaba wa silaha wakati vita vya Russia vinapoingia mwaka wa tatu.

Gavana wa Rostov Vasily Golubey, amesema kwamba shambulizi la ndege zisizokuwa na rubani limesababisha moto uliowaka ukubwa wa mita 200 za mraba, lakini hakuna vifo vimeripotiwa.

Golubev ameripoti saa tano baada ya kuripoti tukio kwanye Telegram, kwamba moto umezimwa.

Forum

XS
SM
MD
LG