Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 02:20

Ukraine imefanya mashambulizi mengine ya Drone kwa Russia


Mfano wa Drone za Russia zilizotunguliwa na jeshi la Ukraine
Mfano wa Drone za Russia zilizotunguliwa na jeshi la Ukraine

Wizara ya Ulinzi ya Russia ilinukuliwa ikisema Drone 158 zimeharibiwa na mifumo ya ulinzi wa anga nchini humo.

Maafisa wa Russia wanasema Ukraine ilifanya mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani-Drone mapema leo Jumapili ikilenga maeneo kadhaa ya nchi hiyo, ikiwemo mitambo ya umeme na mitambo ya kusafisha umeme katika mikoa ya Moscow na Tver.

Wizara ya Ulinzi ya Russia ilinukuliwa na shirika la habari la serikali la Tass, imesema Drone 158 zimeharibiwa na mifumo ya ulinzi wa anga nchini humo. Wizara hiyo imesema kwenye mtandao wa Telegram kwamba idadi kubwa zaidi ya Drone122, zilizotunguliwa katika mikoa ya Kursk, Bryansk, Voronezh na Belgorod, ambayo inapakana na Ukraine. Hakuna uthibitisho huru wa ripoti za Russia.

Pia hakuna maoni ya haraka kutoka Ukraine. Uvamizi huo unakuja siku chache baada ya miundombinu ya nishati ya Ukraine kulengwa na zaidi ya Drone 200 za Russia pamoja na makombora katika moja ya mashambulizi makubwa kama hayo.

Forum

XS
SM
MD
LG