Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 18:33

Ukame waingia tena kaskzini mwa Kenya

Mohamed Mohamud, askari wa wanyama pori kutoka Sabuli akingalia mzoga wa Twiga aliyekufa kutokana na njaa huko katika kijiji cha Matana Kaunti ya Wajirunty, Kenya, Oktoba. 25, 2021.
Mohamed Mohamud, askari wa wanyama pori kutoka Sabuli akingalia mzoga wa Twiga aliyekufa kutokana na njaa huko katika kijiji cha Matana Kaunti ya Wajirunty, Kenya, Oktoba. 25, 2021.

Mizoga ya mifugo iliyonyauka ni ukumbusho kwamba ukame umeingia tena kaskazini mwa Kenya, ikiwa ni hali ya hivi punde zaidi katika mfululizo wa majanga ya hali ya hewa yanayokumba Pembe ya Afrika.

Mizoga ya mifugo iliyonyauka ni ukumbusho kwamba ukame umeingia tena kaskazini mwa Kenya, ikiwa ni hali ya hivi punde zaidi katika mfululizo wa majanga ya hali ya hewa yanayokumba Pembe ya Afrika.

Wakati viongozi wa dunia wakihutubia mkutano wa kilele wa hali ya hewa wa kimataifa huko Glasgow, Scotland wafugaji wanatazama wanyama wao wakiteseka kwa ukosefu wa maji na chakula. Yusuf Abdullahi anasema amepoteza mbuzi 40.

";Ikiwa watakufa, na sisi sote tunakufa," alisema.

Serikali ya Kenya imetangaza janga la kitaifa katika kaunti 10 kati ya kaunti zake 47. Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya watu milioni 2 wana uhaba mkubwa wa chakula. Na huku watu wakienda mbali zaidi kutafuta chakula na maji, watafiti wanaonya kwamba mizozo kati ya jamii inaweza kuongezeka

Wanyamapori wameanza kufa, pia, anasema mwenyekiti wa Hifadhi ya Wanyamapori ya Subuli, Mohamed Sharmarke.

XS
SM
MD
LG