Kwenye ripoti ya kijasusi ya kila siku wizara hiyo imesema kwamba vyombo hivyo vilishtushwa na habari za uasi na vilikuwa havijajitayarisha. Baada ya jaribio hilo kuzimwa, taarifa zimeongeza kusema kwamba vyombo hivyo vilianza kutoa taarifa za kupinga vyombo vingine vya habari, kwamba vikosi vya serikali havikufanya lolote katika kukabiliana na mamluki wa Wagner.
Ripoti hiyo imeongeza kwamba vyombo hivyo vilianza kumpongeza Rais wa Russia Vladimir Putin kwamba alizima jaribio la uasi bila ya umwagikaji wa damu, na vikijitahidi kuliunganisha taifa nyuma ya kiongozi huyo, ambaye tangu uasi huo ulipotokea amekuwa akijitokeza hadharani mara nyingi, kama njia ya kuonyesha umaarufu wake.
Wakati huo huo imeripotiwa kwamba takriban raia 8 wameuwawa huku wengine 13 wakijeruhiwa kutokana na shambulizi la Russia la Jumamosi, kwenye mji wa Ukraine wa Lyman, katika mkoa wa mashariki wa Donetsk.
Forum