Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 10:21

Uhuru wa wanahabari bado changamoto Afrika


Mwanahabari aliyevalia shati lenye maandishi ya kutetea uhuru wa taaluma hiyo ajiunga na wenzake kusherehekea siku ya uhuru wa waaandishi wa habari mjini Kampala, Uganda. Picha na Kennes Bwire.
Mwanahabari aliyevalia shati lenye maandishi ya kutetea uhuru wa taaluma hiyo ajiunga na wenzake kusherehekea siku ya uhuru wa waaandishi wa habari mjini Kampala, Uganda. Picha na Kennes Bwire.

Na waandishi wa VOA

Siku ya waandishi wa habari iliadhimishwa Jumatano katika miji mbali mbali duniani kote, huku wanahabari saba wakiripotiwa kukamatwa nchini Uganda.

Waandishi hao walitiwa mbaroni na polisi baada ya kuzuiliwa kuandaa sherehe kutokana na kuwepo kwa makundi mawili ya uongozi wa wanahabari, kila kundi likishutumu lingine kwa 'uongozi mbovu.'

Kenya pia haikusalia nyuma katika kuadhimisha siku hiyo ya Uhuru wa vyombo vya habari, huku miongoni mwa mada kuu zikijadiliwa wakati taifa hilo likjitayarisha kwa uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti mwaka huu.

Wanahabari wahudhuria mkutano
Wanahabari wahudhuria mkutano

Picha na Kennes Bwire

Hafla iliyoandaliwa mjini Nairobi ilihutubiwa na mwanyekiti wa chama cha waandishi habari cha Kenya, Linus Kaikai ambaye alisema kuwa vyumba vya habari viko tayari kuripoti habari za uchaguzi nchini humo kwa njia fasaha.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na mwenyekiti wa bodi ya kuratibu filamu, Ezekiel Mutua.

Masuala yaliyojadiliwa kwenye mhafla hiyo, ni pamoja na jinsi vyombo vya habari vinanuia kuendeleza uhuru wake na jinsi taasisi za mawasiliano zinavyotakiwa kubuni mikakati thabiti ya kutema habari ghushi au bandia zinazozidisha migogoro, hususan kupitia kwa mitandao ya kijamii.

Nchini Burundi, taaluma ya uandishi wa habari ni kati ya sekta zilizoathiriwa na mzozo unaoisibu nchi hiyo.

Mashirika ya kutetea haki za wandishi wa habari yalisema kuwa bado uhuru wa kutoa habari na haki ya wananchi ya kuzipata bado haziheshimiwi.

Haya yalijiri miaka miwili baada ya vituo vitano vya radio nchini humo kushambuliwa na kuchomwa moto huku nchi hiyo ikiendelea kukabiliwa na mzozo wa kisiasa.

Hata hivyo, mwandishi wa Sauti ya Amerika aliripoti kuwa tatu kati ya radio hizo zilifunguliwa tena na serikali.

Nchini Tanzania, katibu wa chama jukwaa la wahariri, Nevile Meena, aliambia kipindi cha 'Kwa Undani' cha VOA kwamba ukandamizaji wa uandishi wa habari nchini humo unmethiri mno sekta hiyo.

"Hapana shaka kwamba tumepiga hatua, lakini bado kuna vizingiti na visa vingi vya ukandamizaji,' alisema Meena kwa njia ya simu.

Kwingineko ulimwenguni, maandamano yalishuhudiwa katika miji kadhaa huku visa vya kudhulumiwa kwa wanahabari viliripotiwa kuongezeka kufikia mwisho wa mwaka wa 2016.

-Kennedy Wandera, Kennes Bwire na Haidallah Hakizimana walichangia taarifa hiyo.

XS
SM
MD
LG