Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 19:17

Uhuru azindua rasmi mradi wa uzalishaji mafuta Kenya


Raia wa Kenya, Uhuru Kenyatta (Katikati) azindua rasmi awamu ya kwanza ya majaribio ya mradi wa uzalishaji mafuta mjini Lokichar, Kaunti ya Lodwar. Juni 3, 2018.
Raia wa Kenya, Uhuru Kenyatta (Katikati) azindua rasmi awamu ya kwanza ya majaribio ya mradi wa uzalishaji mafuta mjini Lokichar, Kaunti ya Lodwar. Juni 3, 2018.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Jumapili alizindua rasmi awamu ya majaribio ya uzalishaji na usafirishaji wa mafuta ghafi kutoka eneo la Lokichar, kaunti ya Turkana, katika kile alichokitaja kuwa azima ya nchi hiyo ya kujiunga na mataifa mengine ya ulimwengu yanayozalisha bidhaa hiyo.

Wakati wa hafla hiyo, malori manne yaliyobeba mapipa mia mbili ya mafuta ghafi yalianza safari kwelekea kwenye kuituo cha mafuta kilicho mjini Mombasa.

Kwa mujibu wa Rais Kenyatta, mafuta hayo ghafi yanasafirishwa katika awamu ya majaribio, ambapo yatawekwa kwenye kituo hicho cha Mombasa huku serikali ikitafuta wananunuzi wa mafuta kutoka nje.

Kenya imejiunga na Uganda na kuwa nchi ya pili ya Afrika Mashariki kuzalisha mafuta.

Kampuni ya Tullow Oil, iliyopewa kandarasi ya uchimbaji wa mafuta hayo, inatazamia kutoa mapipa 2,000 kila siku.

Kufikia sasa, tayari imetoa mapipa 70,000 ambayo yanaendelea kuhifadhiwa kwenye matangi yaliyo mjini Lokichar.

Kenyatta alisema serikali yake imeweka mikakati ya kisheria, kuhakikisha kwamba wakati bidhaa hiyo itaanza kuuzwa, haitakuwa "laana" walakuleta mvutano kama ulioshuhudiwa katika baadhi ya nchi zilizogundua mafuta katika siku za karibuni.
Mafuta yaligunduliwa katika eneo hilo la Turkana mnamo mwaka wa 2012.

Wiki mbili zilizopita, serikali ilitangaza kwamba sheria ilikuwa imepitishwa kuhusu ugavi wa mapatyo hauyo, ambappo serikali kuu itapata asili mia 75 ya mapato hayo, utawala wa kaunti ukipata asili mia 20, na wenyeji wapate asili mia 5.

Baadhi ya jamii zinazoishi katika maeneo hayo zimekuwa zikilalamika kwamba serikali inanuia kuchukua kiasi kikubwa zaidi cha mapato kutokana na mafuta hayo.

XS
SM
MD
LG