Mabao ya Uholanzi yalifungwa na Memphis Depay katika dakika ya 10, Daley Blind katika dakika za majeruh za kipindi cha kwanza na Denzel Dumfries katika dakika ya 81 ya mchezo.
Bao pekee la Marekani lilifungwa na Haji Wright katika dakika ya 76 huyu ni mchezaji mwenye asili ya Liberia na Ghana na anachezea klabu ya Antalyaspor Kulübü ya Uturuki.Marekani ilipata matokeo kama haya katika michuano ya mwaka 1994, 2010 na 2014.
Timu ya Marekani imeshinda mchezo mmoja tu wa raundi ya mtoano tangu iliporejea Kombe la Dunia mwaka 1990 baada ya kukosekana kwa miaka 40.
Kutolewa huku kutawakatisha tamaa Wamarekani wengi ambao walikuwa na hakika kwamba timu yao ina talanta ya kutosha.
Khazri ajiuzulu kuchezea timu ya taifa
Wakati huo huo mchezaji mkongwe na mshambuliaji hatari wa Tunisia Wahhi Khazri ametangaza kustaafu kucheza soka la kimataifa baada ya Tunisia kutolewa katika michuano ya Kombe la Dunia.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alifunga bao la ushindi walipocheza dhidi ya Ufaransa Jumanne, lakini haikutosha kuwaona wakifuzu kuingia hatua ya mtoano.
Tunisia walikuwa na fursa ya kuingia raundi ya pili kwa dakika chache kutokana na bao la Khazri, lakini hilo likabadilika baada ya Australia kutoka nyuma juu na kufunga bao la pili dhidi ya Denmark.