Uhispania imekuwa nchi ya kwanza ya Ulaya kuiomba mahakama ya Umoja wa Mataifa kujiunga katika kesi ya Afrika Kusini inayoishutumu Israel kwa mauaji ya kimbari huko Gaza.
Afrika Kusini iliwasilisha kesi yake katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki mwishoni mwa mwaka jana. Ilidai kuwa Israel ilikuwa inakiuka mkataba wa mauaji ya halaiki katika mashambulizi yake ya kijeshi ambayo yameharibu maeneo makubwa ya Gaza.
Mahakama hiyo imeiamuru Israel kusitisha mara moja mashambulizi yake ya kijeshi katika mji wa kusini mwa Gaza wa Rafah lakini ikaacha kuamuru sitisho la mapigano katika eneo hilo. Israel haijatii na haonyeshi dalili ya kufanya hivyo.
Forum