Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 12, 2024 Local time: 00:54

Uhasama kati ya India na China hauwezi kumalizika hivi karibuni


Waziri mkuu wa India Narendra Modi (ameangalia kulia) akiwa na rais wa China Xi Jinping (ameangalia kushoto) wakati walikuwa katika mkutano wa BRICS oct 16 2016
Waziri mkuu wa India Narendra Modi (ameangalia kulia) akiwa na rais wa China Xi Jinping (ameangalia kushoto) wakati walikuwa katika mkutano wa BRICS oct 16 2016

Wataalam wanasema kwamba kuna uwezekano mdogo sana wa kupungua kwa uhasama wa kijeshi kati ya India na China licha ya shinkizo la kutaka nchi hizo mbili za Asia kuboresha uhusiano wao.

Uhasama kati ya India na China umeongezeka, maelfu ya wanajeshi wakiwa wameshika doria kwenye mpaka wenye mzozo wa Himalaya, kwa muda wa miaka mitano sasa.

Hata hivyo, biashara kati ya nchi hizo mbili imeongezeka.

Wataalam wanasema kwamba India ina wasiwasi kuhusiana na miradi ya ujenzi wa reli na barabara pamoja na mifumo ya kijeshi inayotekelezwa na China katika Himalaya.

Uhusiano kati ya India na China uliharibika sana baada ya mapambano ya kijeshi ya mwezi Juni 2020.

Tangu wakati huo, karibu wanajeshi 50,000 wenye silaha nzito na ndege za kivita, kutoka pande zote wanashika doria kwenye mpaka wa Himalaya usiokuwa na alama za kutambuliwa kwa urahisi kutofautisha kila upande.

Forum

XS
SM
MD
LG