Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 19, 2024 Local time: 23:10

Uhaba wa umeme kote Cuba


Mwendesha pikipiki katika jengo wakati hakuna umeme kote Cuba. October 18, 2024.
Mwendesha pikipiki katika jengo wakati hakuna umeme kote Cuba. October 18, 2024.

Mfumo wa umeme wa Cuba umefeli kufanya kazi tena Jumamosi asubuhi na kupelekea nchi nzima kubaki katika giza kwa mara ya pili.

Shirika la habari linalomilikiwa na serikali ya Cuba limeripoti kwamba mgumo huo umefeli saa chache baada ya maafisa kuanza kurejesha huduma hiyo.

Mfumo wa umeme wa Cuba ulifeli kuanzia Ijumaa mchana baada ya mojawapo ya mtambo mkubwa zaidi kufeli ghafla na kuacha zaidi ya watu milioni 10 bila umeme.

Shirika la kusimamia umeme halijatoa taarifa zaidi ya kilichosababisha mfumo huo kufeli tena jumamosi, na muda utakaochukuliwa kuhakikisha umeme kurudi.

Serikali ya Cuba imesema ukosefu wa umeme unatokana na mashine zake kuzeeka, ukosefu wa mafuta na kuongezeka kwa mahitaji.

Forum

XS
SM
MD
LG