Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 03:35

Uhaba wa noti mpya Nigeria, serikali imerudisha noti ilizokuwa imeziondoa


Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari akiwa Lagos, Nigeria, Jan. 24, 2023.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari akiwa Lagos, Nigeria, Jan. 24, 2023.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameielekeza benki kuu ya nchi hiyo kuruhusu matumizi ya noti za zamani zilizoondolewa katika soko la fedha kuendelea kutumika sambamba na noti mpya hadi tarehe 10 April mwaka huu.

Noti hizo za naira 200, zitaacha kutumika tarehe 10 mwezi April.

Amesema kwamba noti za naira 500 na 1000 hazitumiki na lazima zirejeshwe Benki Kuu.

Raia wa Nigeria wamepata wakati mgumu kupata pesa kutoka kwenye mashine za ATM kutokana na foleni ndefu na uhaba wa noti mpya huku maandamano yakishuhudiwa katika miji kadhaa.

Nigeria ilianza kutumia noti mpya za naira 200, 500 na 1000 mwaka uliopita.

XS
SM
MD
LG