Serikali ya Uganda na kampuni ya ujenzi ya Uturuki ya Yapi Merkezi walitia saini mkataba wa kujenga sehemu ya reli yenye urefu wa kilomita 272, katika jitihada za kukuza biashara ya kikanda, afisa mmoja wa Uganda alisema Jumatatu.
Mratibu wa mradi wa Reli ya Standard Gauge nchini Uganda, Perez Wamburu, alisema makubaliano hayo ni ya sehemu ya kwanza ya njia ya reli ya umeme iliyopangwa ya kilomita 1,700 na sehemu hiyo itagharimu euro bilioni 2.7.
Ujenzi wake utaanza Novemba, Wamburu alisema.
Mradi huo utaongeza biashara na kupunguza gharama za usafiri, katibu mkuu wa wizara ya kazi ya Uganda, Bageya Waiswa, alisema katika hafla ya kutia saini.
Forum