Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 19:42

Uganda yapiga hatua muhimu ya kuanza uchimbaji mafuta, ujenzi wa bomba.


Rais wa Uganda Yoweri Museveni (kushoto) na rais wa Tanzania John Magufuli (kulia) wakielekea katika mojawapo ya vikao kuhusu ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima hadi Tanga
Rais wa Uganda Yoweri Museveni (kushoto) na rais wa Tanzania John Magufuli (kulia) wakielekea katika mojawapo ya vikao kuhusu ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima hadi Tanga

Kampuni ya kuchimba mafuta ya Tullow imetangaza kumaliza mchakato wa kuuza vitalu vyake kwa kampuni ya Total, na kufunga shughuli zake zote nchini Uganda baada ya miaka 16.

Tullow imesema kwamba imepokea dola milioni 500 Jumanne.

“Tullow inatarajia kupokea dola milioni 75 zaidi wakati maamuzi ya mwisho ya uwekezaji yatakapochukuliwa. Itapokea pia malipo kutokana na mapato ya awali wakati uchimbaji mafuta utakapoanza.” Imesema taarifa ya kampuni ya Tullow kwa vyombo vya habari, immendelea kusema kwamba “kumalizika kwa mchakato huu wa malipo ni hatua inayoambatana na makubaliano yaliyofikiwa Oktoba 21 2020, pia yaliyohusisha namna ya kutekeleza mkataba wa kulipa ushuru, kukabidhi keza vitalu vya kampuni ya Tullow kwa Total na umiliki wa sehemu ya 2 ya machimbo ya mafuta ambayo ilikuwa inasimamiwa na kampuni ya Tullow.”

Serikali ya Uganda iliruhusu kampuni ya Tullow kuuza sehemu yake ya vitalu kwa kampuni ya Total, katika eneo la Albert.

Hatua hiyo ilitoa fursa ya kufanyika maamuzi ya mwisho ya kuanza kwa shughuli ya kuchimba mafuta ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa miaka kadhaa.

Mzozo wa ushuru umesababisha mradi wa kuchimba mafuta nchini Uganda, kukwama tangu mwaka 2016.

Mradi huo unatarajiwa kuiletea Uganda dola bilioni 3.5.

Mnamo mwaka 2019 shughuli hiyo ya kuchimba mafuta ilipata pigo kubwa baada ya kampuni ya Total kusitisha shughuli zake zinazohusiana na ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Haima hadi Tanga Tanzania.

Total ilisitisha shughuli hiyo kutokana na kuvunjika kwa mkataba wa kununua sehemu ya vitalu vya kampuni ya Tullow.

Hata hivyo, kampuni inayomilikiwa na serikali ya China – CNOOC, iliamua kuiuzia Total ya Ufaransa, vitalu vyake.

Kampuni ya Total ilikubali kununua vitalu vya Tullow kwa gharama yad ola milioni 575 na kumaliza mzozo wa ushuru.

Chini ya makubaliano ya sasa, kampuni ya Total imepata haki ya kumiliki asilimia 33.33 katika kila sehemu ya machimbo ya mafuta Pamoja na ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta hayo.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG