Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:27

Uganda yakiri kuwa wanajeshi wake 54 waliuawa katika shambulio la Al-Shabab


Wanajeshi wa Uganda wakiwa kwenye kambi ya kijeshi ya Entebbe, wakibeba jeneza za mabaki ya wanajeshi wa Uganda waliouawa nchini Somalia, Septemba 3, 2015, picha ya Reuters.
Wanajeshi wa Uganda wakiwa kwenye kambi ya kijeshi ya Entebbe, wakibeba jeneza za mabaki ya wanajeshi wa Uganda waliouawa nchini Somalia, Septemba 3, 2015, picha ya Reuters.

Walinda amani 54 wa Uganda waliuawa wakati wanamgambo wa Somalia walipovamia kambi ya kijeshi ya Umoja wa Afrika wiki iliyopita, Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema, wakati wa moja ya mashambulizi mabaya kufanywa na wanamgambo wa Al-Shabaab katika nchi hiyo inayokumbwa na vita.

“Tulipata miili ya wanajeshi 54 waliouliwa, akiwemo kamanda wao.” Museveni alisema katika ujumbe wake kwenye Twitter Jumamosi jioni.

Kiongozi huyo mkongwe alikuwa akizungumza wakati wa mkutano na wanachama wa chama tawala cha National Resistance Movement, ofisi ya rais imeiambia AFP leo Jumapili.

Idadi hiyo ya vifo ni moja ya idadi kubwa sana tangu wanajeshi wa serikali ya Somalia wanaosaidiwa na kikosi cha Umoja wa Afrika kinachojulikana kama ATMIS kuanzisha mashambulizi dhidi ya Al-Shabaab mwezi Agosti mwaka jana.

Lilikuwa pia jambo la nadra kwa nchi inayoshiriki kwenye kikosi cha Umoja wa Afrika kukiri idadi kubwa ya vifo vya wanajeshi.

Al-Shabaab, ambao wamekuwa wakiendesha uasi mbaya dhidi ya serikali kuu dhaifu ya Somalia kwa zaidi ya muongo mmoja, walidai kufanya shambulio hilo la tarehe 26 Mei, wakisema walivamia kambi hiyo ya kijeshi na kuua wanajeshi 136.

Forum

XS
SM
MD
LG