Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 04:38

Uganda yaanza kuchimba mafuta yake wiki hii


Uchimbaji wa mafuta katika kitalu cha Kingfisher, katika mwambao wa ziwa Albert, wilayani Kikuube, magharibi mwa Uganda, Januari 24. 2023.
Uchimbaji wa mafuta katika kitalu cha Kingfisher, katika mwambao wa ziwa Albert, wilayani Kikuube, magharibi mwa Uganda, Januari 24. 2023.

Uchimbaji wa kwanza wa mafuta kibiashara nchini Uganda umeanza wiki hii, ikiwa ni sehemu ya mradi wa dola bilioni 10 wa kuendeleza vinu vya mafuta nchini  Uganda na bomba lenye utata linalokwenda mpaka pwani ya Tanzania.

Serekali inasema imeshughulikia masuala yanayoleta mashaka kuhusu athari za miradi ya mafuta kwa mazingira na kuwahamisha watu.

Hata hivyo, wakosoaji wanasema hatari hizo zinapuuzwa.

Uganda imeanza safari yake ya uzalishaji mafuta kwa kuwasha mtambo wa kuchimba visima Jumanne katika kitalu cha mafuta cha Kingfisher kusini magharibi mwa wilaya ya Kikuube.

Kitalu hicho kinacho endeshwa na shirika la serikali ya China ya National Offshore Oil Corporation (CNOOC), kimegharimu takriban dola bilioni mbili ikiwa ni sehemu ya mradi wa dola bilioni 10 wa kuendeleza hifadhi ya mafuta ya Uganda na kujenga bomba hadi Tanzania.

Mkuu wa Mamlaka ya mafuta ya Uganda, Ernest Rubondo, anasema watachimba visima 31 kwenye kitalu cha mafuta cha Kingfisher, na 10 kati ya hivyo vitakuwa kabla ya kuanza uzalishaji katika kipindi cha miaka miwili.

“Kitalu cha mafuta cha Kingfisher kinakadiriwa kuwa na jumla ya mapipa ya mafuta milioni 560. Kati ya hayo, milioni 190 yanatarajiwa kuzalishwa kwa kipindi cha miaka kati ya 20 hadi 25. Kitalu hiki cha mafuta kinatarajiwa kuwa na kiwango cha juu cha uzalishaji wa mapipa 40,000 kwa siku, kwa miaka mitano.”

Kitalu cha mafuta cha Tilenga nchini Uganda, kinachoendeshwa na kampuni ya Total Energies ya Ufaransa, kinatarajiwa kuzalisha mapipa 190,000 kwa siku.

Uganda pia mwaka huu inaanza ujenzi wa bomba lenye urefu wa kilomita 1,400 hadi bandari ya Tanga, Tanzania, ambapo mafuta hayo yatasafirishwa kwenye masoko ya kimataifa.

Mamlaka inaliita Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki kuwa bomba refu zaidi duniani la joto, ambalo wakosoaji wanasema limewakosesha makazi wanavijiji na kutishia mazingira.

Kitalu cha mafuta cha Kingfisher kina upana kuanzia mwambao wa Ziwa Albert mpaka kilomita tatu ndani ya ziwa.

Wanaharakati wanahofia mafuta yanaweza kumwagika kwenye ziwa au vijiji vilivyo karibu na kuhoji jinsi taka kutoka kwa mradi huo zitakavyo dhibitiwa.

Dickens Kamugisha ni mkurugenzi wa Taasisi ya utetezi ya Afrika ya Utawala wa Nishati (AFIEGO), yenye makao yake makuu Uganda.

Alizungumza na VOA kwa njia ya simu, amesema.

"Tuna takriban kesi saba zinazopinga tathmini ya athari za mazingira kijamii. Serikali ya Rais Museveni imepuuza kuhakikisha kuwa mfumo wa haki unafanya kazi ili kusikiliza na kuhitimisha kesi hizo. Kwa hivyo, tunacho fanya ni kuwafahamisha Waganda kwamba miradi hii ni hatari. Itaathiri kilimo, uvuvi, utalii, namaisha.”

Maafisa wa Uganda wanasema wanakijiji walioacha makazi yao walilipwa fidia na kusisitiza walichukua hatua za kulinda mazingira.

Ruth Nankabirwa ni Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda.

"Tumehakikisha hatuachi chochote bila kuzingatia mahitaji yote ya kimataifa. Kwa sababu tunajua si kila mtu anaitakia Uganda mema, na si kila mtu anaitakia Afrika mema. Kwa hivyo, tutachimba tukijua kuwa tumetunza mazingira, afya na usalama.”

Uganda inakadiria kuwa ina mapipa bilioni 6.5 ya mafuta ghafi chini ya ziwaAlbert, lakini ni mapipa bilioni 1.4 pekee yanayoaminika kupatikana.

XS
SM
MD
LG