Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 20:15

Uganda yapiga hatua katika kuanza kuchimba mafuta


Sampo ya aina ya mafuta ghafi yaliyopatikana Uganda ikionyeshwa mjini Kampala, Jan. 27, 2010.
Sampo ya aina ya mafuta ghafi yaliyopatikana Uganda ikionyeshwa mjini Kampala, Jan. 27, 2010.

Kampuni ya kuchimba mafuta ya Tullow imepata ruhusa kutoka kwa serikali ya Uganda, kuuza mgao wake wa machimbo ya mafuta katika eneo la ziwa Albert kwa kampuni ya Ufaransa ya Total.

Hatua hiyo inatarajia kutoa fursa ya kuanza kwa hatua ya mwisho ya uwekezaji katika kuchimba na kusafirisha mafuta ya Uganda kwa soko la kimataifa, ikiwemo ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta hao kutoka Hoima Uganda hadi Tanga, Tanzania.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, kampuni ya Tullow imesema kwamba serikali ya Uganda na mamlaka ya kukusanya ushuru Uganda - URA, zimefikia makubaliano kuhusu namna ya kulipa ushuru kutokakana na kuuza kwa vifaa vyake kwa kampuni ya Total.

“Waziri wa nishati na maendeleo ya madini wa Uganda ameidhinisha hatua ya kupeana vifaa na mali za Tullow kwa kampuni ya Total pamoja na idhini ya utendaji kazi katika machimbo namba 2,” inesema taarifa ya Tullow, ikiendelea kusema kwamba “kwa sababu masharti yote ya serikali yametimizwa, Tullow inatarajia kumaliza shughuli zake katika muda wa siku chache zijazo na kupokeza idhini ya kufanya kazi kwa Total.”

Kampuni ya Tullow itapokea dola milioni 500 katika hatua ya kwanza na dola milioni 75 maamuzi ya uwekezaji ya mwisho yatakapochukuliwa kuhusu mradi huo wa kuchimba mafuta.

Kampuni ya Tullow pia ina haki ya kupokea sehemu ya pesa zitakazopatikana katika awamu ya kwanza ya uchimbaji mafuta hayo.

Tangu mwaka 2016, Uganda imekuwa ikikumabana na changamoto kadhaa za kisheria, kuhusiana na uchimbaji mafuta yake yanayotarajiwa kuielea dola bilioni 3.5.

Mnamo mwaka 2019 mradi huo wa kuchimba mafuta ulikumbana na changamoto kubwa baada ya kampuni ya Total kujiondoa katika mradi

wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta, kufuatia hatua ya kuvunjika kwa mkataba wa kununua sehemu ya mali za kampuni ya mafuta ya Tullow kwenye mradi wa maendeleo wa Albert.

Kmapuni ya Total ilikubali kununua mali za Tullow nchini Uganda kwa gharama yad ola milioni 575, katika hatua iliomaliza mzozo wa ushuru na serikali.

Katika makubaliano ya sasa, Kampuni ya Total itamiliki asilimia 33.33 katika kila leseni ya kuchimba mafuta katika ziwa Albert, pamoja na mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta hayo.

Kampuni za mafuta zimekuwa zikisubiri makubaliano hayo ili kuanza utekelezaji wa miradi kadhaa ikiwemo kuchimba mapipa 230,000 za mafuta ghafi kila siku katika zaidi ya machimbo 500.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA,Washington DC

XS
SM
MD
LG