Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:57

Uganda: Madai ya jeshi letu kuunga waasi wa M23 ni ndoto za mchana


Waandamanaji wa DRC wakiwa wamebeba jeneza na bango lenye picha za rais wa Rwanda Paul Kagame na Uganda Yoweri Museveni. Waandamanaji wanadai kwamba Uganda na Rwanda zinaunga mkono waasi wa M23 Okt 31, 2022
Waandamanaji wa DRC wakiwa wamebeba jeneza na bango lenye picha za rais wa Rwanda Paul Kagame na Uganda Yoweri Museveni. Waandamanaji wanadai kwamba Uganda na Rwanda zinaunga mkono waasi wa M23 Okt 31, 2022

Serikali ya Uganda imefutilia mbali ripoti kwamba inaunga mkono kundi la waasi la M23 ambao wanashikilia sehemu za mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Uganda imesema kwamba uhusiano wake na Jmahuri ya kidemokrasia ya Congo ni mzuri.

“Uhusiano wet una jeshi la Congo – FARDC, na rais wa DRC na baraza lake la mawaziri ni mzuri,” inasema taarifa ya msemaji wa serikali ya Uganda Ofwono Opondo.

Taarifa ya Uganda imetolewa baada ya amseneta wa DRC, makundi ya kutetea haki za kijamii na waandamanaji kudai kwamba Uganda ilikuwa inashirikiana na Rwanda kutatiza usalama wa DRC yenye utajiri mkubwa wa madini.

Kupitia kwa muungano wa jukwaa la mabadiliko, wabunge nchini DRC walitoa taarifa kwa vyombo vya habari ijumaa, wakitaka Kinshasa kumfukuza balozi wa Uganda nchini DRC na kufunga mpaka kati ya nchi hizo mbili kutokana na kile wanaamini kwamba Uganda inaunga mkono waasi wa M23.

Wabunge na mashirika ya kiraia wanataka mpaka ufungwe

Hayo yanajiri siku chache baada ya DRC kumfukuza balozi wa Rwanda Vincent Karega, kutokana na kile DRC inasema kwamba “Rwanda imetuma maelfu ya wanajeshi wake nchini DRC kusaidia waasi wa M23 kupigana na wanajeshi wa serikali ya Kinshasa.”

Taarifa ya wabunge wa DRC hata hivyo haina ushahidi wowote wala kunukuu chanzo cha madai yao kwamba Uganda inaunga mkono waasi wa M23.

Msemaji wa serikali ya DRC Patrick Muyaya aliambia waandishi wa habari wiki hii kwamba serikali ya DRC “inachunguza madai ya Uganda kuunga mkono waasi wa M23”.

Mapema wiki hii, waandamanaji wenye mabango ya kudai kwamba Uganda na Rwanda zinaunga mkono waasi wa M23, waliandamana hadi kwenye mpaka wa DRC na Rwanda kabla ya kutawanywa na maafisa wa usalama wa DRC.

M23 walipokelewa na Uganda mwaka 2013

Mnamo mwaka 2013, wakati wa mapiganao makali kati ya maafisa wa Usalama wa DRC na wanajeshi wa SADEC, waasi wa M23 walikimbilia Uganda na kupewa hifadhi na serikali ya Uganda.

Waliishi katika kambi ya jeshi la Uganda ya Bihanga na kupewa ulinzi mkali kwa muda, kabla ya kurudi DRC wakati wa utawala war ais Joseph Kabila.

Msemaji wa Uganda Ofwono Opondo amesema kwamba Uganda haingesaini makubaliano ya ushirikiano kuhusu ujenzi wa barabara na kuimarisha usalama kupambana na waasi wa Allied democratic forces ADF, iwapo Uganda inaunga mkono waasi wa M23.

“Hata tulikuwa msitari wa mbele katika mazungumzo ya kundi la M23 kuwa sehemu ya jeshi la DRC.”

Ujenzi wa barabara ya kutoka Bunagana hadi Goma umesitishwa tangu kundi la M23 lilipodhibithi mji wa Bunagana mapema mwaka huu.

‘Ndoto za mchana’

Wanajeshi wa Uganda wakiwa katika oparesheni, Beni, DRC Dec. 8, 2021.
Wanajeshi wa Uganda wakiwa katika oparesheni, Beni, DRC Dec. 8, 2021.

Msemaji wa jeshi la Uganda Brig Jenerali Felix Kulayigye, amesema kwamba waasi wa M23 walijaribu kuchoma moto magari na vifaa vyaujenzi wa barabara hiyo mjini Bunagana.

“Wamejaribu kuchoma moto vifaa vya ujenzi. Ninaposikia madai kwamba tunaunga mkono waasi wa M23, nakasirika sana,” amesema Kulaigye.

Vifaa hivyo vya ujenzi vimerudishwa Uganda.

Ujenzi wa barabara hiyo, uliokuwa unatekelezwa na kampuni ya Dott services, ulitarajiwa kuharakisha usafirishaji wa bidhaa kutoka Uganda hadi mji wa Goma na kuimarisha biashara kati ya Goma na Kampala.

Barabara hiyo ya Bunagana, Ruchuru hadi Goma ni ya urefu wa Kilomita 89.

Waseneta wa DRC wamedai kwamba wanajeshi wa Uganda waliwasaidia waasi wa M23 hivi karibuni, kuwashinda nguvu wanajeshi wa DRC katika mapigano ya kudhibithi Bunagana, madai ambayo msemaji wa jeshi la Uganda Felix Kulayigye amesema “wanaota ndoto ya mchana”

XS
SM
MD
LG