Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 07:37

Uganda kusitisha uagizaji wa bidhaa za mafuta kupitia bandari ya Mombasa


Kinu cha mafuta magharibi mwa Uganda kinachendeshwa na China.
Kinu cha mafuta magharibi mwa Uganda kinachendeshwa na China.

Waziri wa nishati wa Uganda amesema Alhamisi kwamba nchi yake inafanya mashauriano na Tanzania, juu ya kuagiza bidhaa zote za mafuta kupitia bandari ya Dar es Salaam, ikiwa na maana ya kwamba huenda ikasitisha kutumia bandari ya Mombasa nchini Kenya.

Uganda haijakuwa inaridhishwa na mfumo wa muda mrefu ambapo makampuni ya mafuta ya Uganda yalikua yananunua asilimia 90 ya bidhaa za mafuta kupitia matawi ya makampuni yaliopo Kenya.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni alilalamikia mpango huo akisema kwamba unaathiri usafiri wa bidhaa kuelekea nchi yake, pamoja na kusababisha gharama za juu za mafuta. Kwa kukabiliana na hali hiyo alitangaza mwezi Novemba mwaka jana, kwamba Uganda imeipatia haki pekee ya kuagizia bidhaa zake zote za mafuta, kitengo cha kampuni ya nishati ya kimataifa ya Vitol.

Uganda iliagiza bidhaa za mafuta zenye dhamani ya dola bilioni 1.6 hapo 2022, nyingi zikitokea kwenye mataifa ya ghuba. Waziri wa nishati Ruth Nankabirwa alisema kwamba nia ya Uganda ilikuwa kuendelea kuingizia bidhaa zake Mombasa, lakini serikali ya Kenya ilikataa kutoa leseni zinazohitajika, suala ambalo limepelekea mashauriano na serikali ya Tanzania.

Forum

XS
SM
MD
LG