Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 08, 2024 Local time: 22:24

Ufaransa yaunga mkono mpango wa Morocco kuhusu Sahara Magharibi


Mwanajeshi wa Polisario Front akitoa salamu wakati wa gwaride la kijeshi kusherehekea kumbukumbu ya miaka 50 ya Polisario Front katika kambi ya Aoussered, Algeria Mei 20, 2023.
Mwanajeshi wa Polisario Front akitoa salamu wakati wa gwaride la kijeshi kusherehekea kumbukumbu ya miaka 50 ya Polisario Front katika kambi ya Aoussered, Algeria Mei 20, 2023.

Ufaransa inatambua mpango wa kujitawala kwa eneo la Sahara Magharibi chini ya mamlaka ya Morocco kama njia pekee ya kutatua mzozo wa muda mrefu kuhusu eneo hilo, Rais Emmanuel Macron alisema katika barua yake siku ya  Jumanne.

Mgogoro huo, ulioanzia mwaka 1975, unaingiza Morocco, ambayo inaichukulia Sahara Magharibi kuwa eneo lake, dhidi ya Polisario Front inayoungwa mkono na Algeria, ambayo inatafuta kuwa na taifa huru huko.

Ufaransa, kama utawala wa zamani wa kikoloni katika eneo hilo, imepitia mivutano ya kidiplomasia kati ya Rabat na Algiers kuhusu suala hilo. Washirika wengi wa Ufaransa, nchi za Magharibi tayari wanaunga mkono mpango huo wa Morocco.

"Kwa Ufaransa, uhuru chini ya mamlaka ya Morocco ndio mfumo ambao suala hili lazima litatuliwe," kwa mujibu wa barua iliyotumwa na Macron kwa Mfalme wa Morocco Mohammed VI.

Forum

XS
SM
MD
LG