Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 04:56

Ufaransa, Ujerumani, Ubelgiji zimeagiza Rwanda kuacha kusaidia M23


Rais wa Rwanda Paul Kagame
Rais wa Rwanda Paul Kagame

Serikali ya Rwanda inaendelea kukabiliwa na shinkizo la kimataifa, kwa shutuma za kutoa msaada wa kijeshi kwa kundi la waasi la M23 linalopigana na wanajeshi wa serikali mashariki mwa Jamhuri ya kidemkrasia ya Congo.

Ufaransa na Ujerumani ni nchi za hivi punde ambazo zinaitaka Rwanda kuacha kuwasaidia waasi hao, na kuonya kuchukua hatua kali ikiwemo kusitisha msaada wa kifedha kwa utawala wa Rwanda ambao umekuwa ukitolewa kwa muda mrefu.

Mapigano ya waasi wa M23 yamekuwa yakiendelea mashariki mwa DRC, kwa muda wa miezi kadhaa sasa.

Ripoti ya wataalam wa umoja wa mataifa iliyotolewa mapema mwaka huu ilisema kwamba kuna ushahidi wa kutosha kwamba serikali ya Rwanda inaunga mkono waasi hao, na Marekani imeitaka Rwanda kuacha kutoa msaada kwa waasi hao.

Sasa, wafadhili wakubwa wa Rwanda wameitaka Rwanda kuacha kuwasaidia waasi wa M23.

Wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa imetoa taarifa inayoshutumu msaada wa Rwanda kwa waasi hao

Msaada wa Ufaransa kwa Rwanda umeongezeka kutoka dola milioni 4 mwaka 2019 hadi dola milioni 68 mwaka 2021.

Mkuu wa shughuli katika wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani, katika jangwa la Afrika Christoph Retzlaff, ameandika ujumbe wa Twitter akisema kwamba Rwanda inastahili kuacha kutoa msaada wake kwa kundi la M23 mara moja na kuchangia kikamilifu kutafuta suluhu kwa mgogoro mbaya nchini DRC.

Ujerumani ilitoa msaada wa dola milioni 94 kwa Rwanda, mwaka 2021. Ubelgiji ambayo ilikuwa utawala wa kikoloni wa Rwanda, vile vile imeelezea msimamo huo. Serikali ya Rwanda imeendelea kukana madai kwamba inawaunga mkono waasi wa M23 na kushutumu jumuiya ya kimataifa kwa kukataa kukabiliana na sababu kubwa ya matatizo yaliyo mashariki mwa DRC ambapo kuna zaidi ya akundi ya waasi 100.

XS
SM
MD
LG