Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 07:00

Europol yasema udukuzi umeathiri nchi 150


Picha hii inaonyesha tovuti ya NHS inayowatahadharisha watu kuhusu udukuzi huo nje ya Wizara ya Afya nchini Uingereza
Picha hii inaonyesha tovuti ya NHS inayowatahadharisha watu kuhusu udukuzi huo nje ya Wizara ya Afya nchini Uingereza

Uvamizi wa kutisha wa udukuzi wa mifumo ya kompyuta (Cyberattack) tayari umeathiri nchi 150 na kunauwezekano ukaongezeka Jumatatu.

Tahadhari hiyo imetolewa wakati watu wakirejea makazini baada ya wikiendi na pengine watapoanza kutumia kompyuta ambazo pengine hazijawekewa upya ulinzi dhidi ya virusi.

Idara ya polisi ya Europol imesema Jumapili shambulizi hilo tayari lilikuwa limeathiri sio chini ya taasisi 100,000 katika nchi 150, wakati mifumo ya takwimu iliokuwa imedukuliwa na kirusi cha malware kinachofunga mafaili ya computer mpaka mtumiaji alipe fidia.

“Na wasiwasi jinsi idadi hiyo itakavyo endelea kuongezeka wakati watu wakirudi makazini na kufungua kompyuta zao Jumatatu,” Mkurugenzi wa Europol Rob Wainwright amekiambia kituo cha televisheni cha Uingereza ITV.

Mpaka sasa hivi hakuna habari yoyote ilipatikana katika juhudi ya kujua nani aliyeanzisha shambulizi hili la udukuzi.

Wataalamu wa usalama wa mifumo ya kompyuta wamewahakikishia watumiaji wa kompyuta ambao walikuwa wamehakikisha kuwa wamejadidisha mifumo ya “PC operating systems” watakuwa wamenusurika lakini wamesisitiza kuwa kampuni na serikali wahakikishe wanaweka ulinzi katika kompyuta au wanaingiza mifumo mipya ya ulinzi.

Wataalamu wameshauri kuwa wale wote ambao mitandao yao ilifungwa na kirusi kinachojulikana kama ransomware wasifanye malipo yoyote waliotakiwa na wahalifu hao wa mitandao, ambazo ni Dola za Kimarekani 300.

Hata hivyo watayarishaji wa kirusi hicho cha kidukuzi cha “WannaCry” ransomware chenye kufanya mashambulizi wamewaambia waathirika wake kiwango cha fedha kitaongezeka maradufu iwapo hawatofuata maelekezo katika siku tatu tangu udukuzi huo utokee- ikiwa ni Jumatatu kwa wengi walioathiriwa.

Aidha wadukuzi hao wameonya kuwa iwapo watu hawatotii amri yao watafuta mafaili yote katika mfumo wa kompyuta hizo zilizoathirika iwapo malipo hayatofanyika katika kipindi cha siku saba.

Avast, ambayo ni kampuni inayotengeneza 'software' za ulinzi imedai kuwa inawatumiaji milioni 400 duniani, na imesema imebaini kirusi hicho cha ransomware kilichoshambulia, kiliongezeka kwa kasi siku ya Jumamosi kufikia dukuzi 57,000.

Avast ambayo iliasisiwa mwaka 1988 na watafiti wa Czech, imesema idadi kubwa ya udukuzi huo uliilenga Russia, Ukraine na Taiwan, lakini taasisi kubwa katika nchi nyingi duniani ziliathirika pia.

XS
SM
MD
LG