Serikali ya Hong Kong ilikuwa ikihangaika na kampeni za mwisho za wagombea siku ya Jumapili kujaribu kuongeza idadi ya watu kujitokeza katika uchaguzi uliofanyiwa marekebisho mapya wa wabunge wazalendo pekee, ambao ni wa kwanza chini ya sheria mpya ya usalama.
Baada ya saa nane za kupiga kura, waliojitokeza kupiga kura walikuwa zaidi ya asilimia 10 chini ya kiwango cha uchaguzi uliopita wa Baraza la bunge miaka mitano iliyopita.
Uchaguzi huo ambao ni wagombea pekee waliochujwa na serikali kama wazalendo ndio wanaweza kugombea umekosolewa na baadhi ya wanaharakati, serikali za nje na makundi ya kutetea haki huku vyama vikuu vinavyounga mkono demokrasia havishiriki.