Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 09, 2024 Local time: 10:30

Uchaguzi wa Venezuela ulikumbwa na 'udanganyifu mkubwa'


Maandamano yanaendelea Puerto La Cruz kupinga ushindi wa rais Nicolas Maduro July 29 2024
Maandamano yanaendelea Puerto La Cruz kupinga ushindi wa rais Nicolas Maduro July 29 2024

Wakati maandamano yanaendelea kote nchini Venezuela kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika Jumapili, kituo cha Marekani cha Carter, kimesema uchaguzi huo uliomalizika kwa ushindi wa rais Nicolas Maduro, hauwezi kutambuliwa kuwa wa kidemokrasia.

Shirika hilo lisilo la kiserikali, lililoanzishwa na rais wa zamani Jimmy Carter, lilituma wataalam 17 wa uchaguzi katika nchi hiyo ya Amerika Kusini kufuatilia uchaguzi huo.

Katika taarifa iliyotolewa Jumanne, kituo cha Carter kimesema kwamba uchaguzi huo haukufikia viwango vya kimataifa.

Baraza la uchaguzi la Venezuela, ambalo linadhibitiwa na Maduro, lilitangaza mapema Jumatatu kwamba rais Maduro alishinda uchaguzi kwa asilimia 51. Mshindani wake Edmundo Gonzalez, amepata asilimia 44.

Matokeo hayo yanatofautiana sana na ukusanyaji maoni uliofanywa baada ya uchaguzi kufanyika ulioonyesha kwamba Gonzalez alikuwa anaelekea kupata ushindi mkubwa.

Forum

XS
SM
MD
LG