Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:34

Uchaguzi wa Burundi unafikisha ukingoni utawala wa mihula mitatu ya Nkurunziza


Kampeni zilizomalizika mwishoni mwa wiki ziligubikwa na ghasia kati ya wafuasi wa vyama vikuu viwili chama tawala cha CNDD FDD na kile kikuu cha upinzani cha CNL, na kuzusha hofu ikiwa uchaguzi utafanyika kwa amani na haki.

Uchaguzi wa Burundi unatazamiwa kuleta mabadiliko ya uchumi na uwongozi
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:35 0:00

Mgombea kiti cha rais wa chama kikuu cha upinzani cha CNL, Agathon Rwasa ameiambia Sauti ya Amerika kwamba, anashiriki kwenye uchaguzi licha ya kasoro zizliopo ili kuweza kuleta mabadiliko, lakini hofu yake kubwa ni ukosefu wa wakilishi wao kwenye vituo vya kupiga kura kuweza kujua ikiwa ni utaratibu wa haki na vipi kuhakikisha.

Agathon Rwasa akizungumza kwenye mkutano mkuu wa chama chake cha Congres National pour la Liberte, CNL
Agathon Rwasa akizungumza kwenye mkutano mkuu wa chama chake cha Congres National pour la Liberte, CNL

"Uchaguzi unaweza kua wa huru na haki"

Katika uchaguzi wa rais kuna wagombea 7 wanaotaka kuchukua nafasi ya Pierre Nkuruziza ambae anatajwa sasa kama kiongozi mkuu wa taifa.

Hali hiyo inasababisha wachambuzi kuuliza ikiwa kweli aatapenda kuona chama tawala cha CNDD-FDD kinaondoka madarakani.

Makamu rais Gaston Sindimwo ambae ni moja wapo ya wagombea kiti cha rais kwa niaba ya chama cha UPRONA ana hofu ikiwa uchaguzi utakua wa huru ukichukulia jinsi kampeni zilivyogubikwa na ghasia.

Licha ya kuwepo na wagombea hao 7 wagombea wawili ndio wanaotajwa zaidi nao ni mgombea wa chama tawala cha CNDD FDD Evariste Ndayshimiye mgombea mkuu wa upinzani na Agathon Rwasana wa chama cha CNL.

Kila maja anadai atapata ushindi na hapo kuzusha hoja ikiwa mmoja akishinda mwengine atakubali matokeo au kunaweza kutokea vurugu tena. Rwasa anasema ikifika hali kwamba wanashindwa atafuata mkondo wa sharia.

Evariste Ndayishimiye, kushoto, akiwa pamoja na rais Pierre Nkurunziza, kulia, baada kuteuliwa mgombea wa chama cha CNDD-FDD…
Evariste Ndayishimiye, kushoto, akiwa pamoja na rais Pierre Nkurunziza, kulia, baada kuteuliwa mgombea wa chama cha CNDD-FDD…

Mgombea kiti wa chama tawala aliyeteuliwa na Nkuruziza, Jenerali aliyestahafu Evariste Ndayshimiye, ambae hakujibu ombi letu la khojiana nae, akifunga mkutano wake wa kampeni jumamosi amewashukuru wafuasi wake na wagombea wenzake kwa kuendesha kampeni iliyokua na ushindani mkubwa.

“Nawashukuru wote walioniamini, wale ambao wako katika vyama na wasiokua ndani ya vyama. Nawashukuru pia washindani wangu ambao walijitahidi kuvumiliana, na kuvumilia wengine, Wenye hisia tofauti na zao. Tunawaomba waendelee na uvumilivu, wawashauri wafwasi wao."

Akiwa anataka kuchukua nafasi ya aliyemtanguliwa Ndaysimiye anakabiliwa na changamoto kubwa ya kufuta tuhuma za ukiukaji wa haki za binadam na mateso yaliyotendwa chini ya utawala wa Nkurnziza.

Tuhuma ambazo zimetolewa mara kwa mara na Umoja wa Mataifa na mashirika ya kutetea haki za binadam na hata serikali kuwafukuza wajumbe wa tume ya haki za binadam ya umoja wa mataifa.

Mgombea wa CNDD FDD anasema atafanya mageuzi katika mfumo wa sharia ili kuhakikisha haki inatendeka.

Licha ya ahadi hiyo, suala linabaki juu ya ikiwa kweli uchaguzi utafanyika kwa njia ya huru na haki hasa kwa vile uchaguzi huu utafanika bila ya kuwepo wafuatiliaji wa kimataifa.

Serikali ya Bujumbura imekata kuwaruhusu wafuatiliaji kutoka Umoja wa Afrika AU, na Umoja wa Mataifa ikidai AU inaunga mkono upinzani. Na Jumuia ya Afrika ya Mashariki haikuweza kupeleka maafisa wao kwani Bujumbura iliwataka wabaki karantin kwa siku 14, hivyo hawataweza kufanya kazi zao kwa muda unaostahiki.

Emery Pacifique Igiraneza, kiongozi wa shirika linalojumuisha raia wa Burundi waishio ugenini linalotetea uongozi bora( MAP Burundi). Anasema hamaini kwamba uchaguzi utakua huru na wa haki.

Hakuna takwimu za uchunguzi wa maoni kuweza kufahamu nani kwa hakika nani anaongoza miongoni mwa wapiga kura, lakini wachambuzi wanasema ukiangalia idadi ya wafuasi walohudhuria mikutano ya kampeni unaona kwamba ushindani uko kati ya mgombea kiti wa chama tawala Ndaiyshimiye na Yule wa upinzani Rwasa.

Ni matumaini ya kila mtu uchaguzi ufanyika kwa amani na salama.

XS
SM
MD
LG