Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:03

Ubalozi wa Marekani nchini Zimbabwe unasema uchaguzi haukukidhi viwango vya katiba ya nchi hiyo


Watu wanatafuta majina yao, nje ya kituo cha kupigia kura mjini Harare, Agosti 24, 2023
Watu wanatafuta majina yao, nje ya kituo cha kupigia kura mjini Harare, Agosti 24, 2023

Ubalozi wa Marekani mjini Harare umejiunga na waangalizi wengine wa uchaguzi kuelezea wasi wasi wao kuhusu uchaguzi mkuu wa Zimbabwe, ukisema haukufikia viwango vya katiba ya nchi hiyo na miongozo ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika.

Uchaguzi mkuu wa Zimbabwe siku ya Jumanne haukukidhi viwango vya kimataifa , Rebecca Archer-Knepper, kaimu msemaji wa Ubalozi wa Marekani mjini Harare, aliiambia VOA Jumamosi, lakini alisema Washington ina matumaini kuwa Wazimbabwe watabakia kuwa na amani wakati tume ya uchaguzi inahesabu kura.

“Wakati siku za uchaguzi zilikuwa za amani, mchakato wa uchaguzi hadi hivi sasa haujakidhi viwango vya kikanda na kimataifa, tunashirikiana wasi wasi wetu mkubwa sana kama ule ambao umeelezewa na SADC na ujumbe wa waangalizi wengine wa kimataifa. Taarifa ya SADC ya Agosti 25 ilielezea kuwa uchaguzi ‘haukukidhi mahitaji ya Katiba ya Zimbabwe, Sheria ya Uchaguzi, na Misingi na Miongozo ya SADC inayotawala Kanuni za Kidemokrasia katika Uchaguzi,” amesema balozi Archer-Knepper.

Mwanadiplomasia huyo wa Marekani ameongezea kuwa “tume hizi zimeelezea matatizo kwa uwazi, uhuru, haki na hadhi ya mchakato wa uchaguzi; masharti yasiyofaa juu ya haki ya uhuru wa kukutana na kushirikiana, na uhuru wa kujieleza mambo ambayo yameelezewa kwenye katiba ya Zimbabwe; na kuwaengua wagombea, hasa wanawake. Pia tuna wasi wasi mkubwa sana wa kukamatwa kwa wanachama wa mashirika ya kiraia ambao tunaamini walikuwa wakifanya shughuli zao kisheria, bila ya kuegemea upande wowote katika kazi ya uangalizi wa uchaguzi.”

Siku ya Jumatano, polisi waliwakamata waangalizi 35 wa uchaguzi kutoka Zimbabwe Election Support Network and Election Resource Center na kuwaweka ndani na kuwashtaki kwa njama za kutangaza matokeo yasiyo rasmi, waliachiliwa kwa dhamana ya dola 200 kila mmoja siku ya Ijumaa.

Wasimamizi wa uchaguzi wakiwemo wale wa SADC wamelaani ukamataji huo na kuzuia kompyuta za waangalizi hao na simu zao za mkononi, kulikofanywa na polisi, pamoja na jinsi uchaguzi ulivyoendeshwa.

Siku ya Ijumaa, Christopher Mutsvangwa, msemaji wa chama tawala wa ZANU-PF aliwajibu waangalizi wa SADC kuhusu ukosoaji wao kwa uchaguzi.

“Sasa, ukija katika misingi ya SADC, tunataka kuweka bayana, kuwa ni matokeo ya mataifa wanachama wa SADC. Hayatekelezwi na kila mwanachama binafsi ambaye anakuwa mkuu wa ujumbe. Si wajibu wa mtu fulani maalum kujitwika mwenyewe jukumu la kutathmini kamati ya katiba ya sheria za Zimbabwe. Kwa hiyo Bwana Nevers Mumba kutoka Zambia, tunakueleza wewe. Usiingilie sheria za Zimbabwe,” alisema Mutsvangwa.

Nevers Mumba, mkuu wa tume ya uangalizi ya SADC kwa uchaguzi wa Zimbabwe, alisita kusema kuwa uchaguzi mkuu si wa kuaminika wakati alipowasilisha ripoti ya awali ya umoja huo siku ya Ijumaa, lakini alielezea wasi wasi wao.

Raia huyo wa Zambia alisema ada ya dola 20,000 ya kujiandikisha kuwa mgombea uraia ilikuwa ni kubwa mno, alielelezea pia kuhusu Tume ya Taifa ya uchaguzi ya Zimbabwe kusita kutoa orodha ya wapiga kura kwa upinzani kwa muda muafaka na kukosoa kuvurugwa kwa mikutano ya uchaguzi ya wapinzani kulikofanywa na polisi.

Waziri wa Sheria wa Zimbabwe, Ziyambi Ziyambi alielezea uungaji mkono wake kwa taarifa za Mutsvangwa.

Forum

XS
SM
MD
LG