Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 21, 2024 Local time: 00:48

Udadisi wa kijana mweusi aliyekuwa analelewa na wazungu


Angela Tucker and her adoptive mom, Teresa Burt, pause during a walk on the Bellingham waterfront. (Claire Morin-Gibourg/VOA)
Angela Tucker and her adoptive mom, Teresa Burt, pause during a walk on the Bellingham waterfront. (Claire Morin-Gibourg/VOA)

Angela Tucker ambaye wakati anakua akijihisi hajakamilika, hata akiwa ndani ya familia kubwa ya ndugu saba, baadhi yao wazungu, baadhi weusi, wengi wao wamechukuliwa kulelewa.

Alipokuwa na umri wa miaka 26, aligundua kuwa mama yake mzazi, alimsaidia kujihisi kuwa amekamilika, amesema.

Hivi sasa akiwa na miaka 33, anasaidia katika huduma za watu wanaotaka watoto wa kuwalea huko Seattle katika ofisi ya Amara, anazungumzia yeye kama mmoja wa waliolelewa na kuwasaidia watoto wadogo kujijenga na kujifahamu vyema.

Tucker katika kuwatafuta wazazi waliomzaa alipata msaada mkubwa kutoka kwa watu waliomlea Teresa na David Burt.

“Ilikuwa vigumu sana kwangu mimi kwanza, kwa sababu nilihisi pengine yeye kukutana na mama yake mzazi ingekuwa kama vile anatafuta mzazi mbadala,” Teresa Burt alisema. Lakini anasema mtoto wake alimbadilisha mawazo yake, na kumuwezesha kuwa sehemu ya hiyo azma ya kutaka kumuona mama mzazi na ilikuwa ni hamasa kubwa. Kwa kweli ilinifanya nijisikie niko huru.”

David Burt anasema hakuhisi chochote, hakuwa na khofu kwamba azma ya Angela huenda ingedumaza uhusiano wake na mtoto wake wa kike.

‘’Nilipata furaha ya kumlea tangu alipokuwa na umri wa mwaka mmoja mpaka alipongia chuoni. Sikupoteza chochote,” amesema.

Tucker alimpata baba yake mzazi kwanza na halafu mama yake mzazi, Deborah takriban, muongo mmoja uliopita. Anazungumza na kuwasiliana naye mara kwa mara.

Deborah anasema kuwasiliana na mwanawe ilikuwa ni kama “zawadi kutoka kwa Mungu.”

Tucker bado hana majibu kwa maswali yote anayomuuliza Deborah. Mwanamke kijana anakiri kwamba tofauti za maisha ikiwa ni pamoja na fursa ya elimu nzuri na kiuchumi juu ya Deborah ni kikwazo. “hivyo, anadhani kwamba mawasiliano ni magumu kutokana na hilo.”

Yeye na Deborah wanapendana, na wana mawasiliano ya karibu, lakini wanaishi kitofauti kabisa,” amesema Tucker.

Teresa Burt anasema mtoto wake kumtafuta mzazi wake kumemfanya kuwa na nguvu zaidi. Baada ya kufanya hivyo, anaweza kuwasaidia wengine na hivi sasa anasaidia wengine kutafuta wazazi wao.”

Tucker amefungua tovuti ambayo inazungumzia yale aliyoyapitia na kuweka mfululizo wa visa kwa msaada wa mume wake ambaye ni mtengenezaji filamu, Bryan Tucker. Humo kuna makala inayoitwa “The Adopted Life” kwenye http://www.theadoptedife.com/episodes Anazungumza ana kwa ana na vijana ambao wanalelewa na walezi, na kutumia ujuzi wake huko Amara, ambao ameanza kuwaingiza katika program maalum ya ushauri.

Mmoja wa wale ambao wanalelewa na walezi ambao si wazazi wao kibaiolojia ni Maggie, ana umri wa miaka 9 ni mtoto wa Amy na Brett Bowton-Meade. Wawili hao, ambao ni wazungu, pia wana watoto wawili wa kike ambao ni wa kuwazaa.

Maggie amekuwa akijitahidi kujibu maswali kuhusu anahusika wapi na mama yake mzazi yuko wapi. Tucker, mshauri wake, amemtia moyo kuweka rekodi ya kila kitu.

“Nimekuwa nikiandika kila kitu katika kitabu changu,” Maggie amesema, akielezea kwamba kitabu hicho pia kina picha. “Kama nitakutana naye siku yoyote, nitakwenda nacho.”

Akiwa kazini, Tucker anajaribu kurahisisha utaratibu wa kuasili watoto, ikiwemo kusukuma mawazo kama vile kuzishawishi familia za watu weusi nao kuchukua watoto kuwalea.

“Sisemi kwamba kuasili kuwe tu kwa watu rangi fulani. Lakini ninachosema ni kama vile unatembea katika mstari mwembamba sana,” amesema.

Tangu awapate wazazi wake, Tucker anasema anahisi, “Hana mkanganyiko tena. Lakini ukweli ni kwamba mama yake mzazi hakuweza kumlea ni jambo la kusikitisha. Na hilo halitabadilika.

XS
SM
MD
LG