Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 08, 2024 Local time: 03:19

Tuzo za Oscar 2019 : Filamu ya Green Book yashinda tuzo tatu


Amatus Sami-Karim, kushoto na mumewe Mahershala Ali wakiwasili katika tamasha la Oscar, Februari 24, 2019.
Amatus Sami-Karim, kushoto na mumewe Mahershala Ali wakiwasili katika tamasha la Oscar, Februari 24, 2019.

Tamasha la tuzo za Oscar za 91 zilifana usiku wa Jumapili katika jiji la Los Angeles kwenye jimbo la California.

Green Book, filamu yenye kusisimua inayohusu urafiki kati ya mwanamuziki Mmarekani mweusi na dereva wake mzungu ambaye siyo mstaarabu, ikisimulia hali ilivyokuwa wakati wa kipindi cha ubaguzi nchini Marekani, imeshinda tuzo tatu za Academy ikiwemo katika kundi la Picha Bora.

Tuzo hiyo iliyokuwa ikitarajiwa sana imekuwa muwafaka katika usiku uliyokuwa umewakutanisha watu wa rangi mbalimbali katika Tamasha la Oscar.

Muigizaji Mahershala Ali wa filamu ya Green Book, ambaye alikuwa anaigiza nafasi ya Don Shirley, alishinda tuzo ya Oscar ya muigizaji msaidizi bora. Filamu hiyo pia imeshinda tuzo ya Oscar ya uandishi wa asili wa filamu uliyo bora.

Filamu ya Green Book licha ya kupata ukosoaji wa hapa na pale ilishinda kipengele cha picha bora 2019 kwa kazi nzuri waliyoifanya katika filamu hiyo ndani ya Hollywood mwaka 2018.

Kipengele cha picha bora kilishirikisha filamu nane ambazo baadhi yake zilipewa kipaumbele cha juu na kuchukuwa tuzo hiyo ikiwemo Black Panther au Roma, ambazo zilikuwa na ushawishi mkubwa. Watu wengi walikuwa wanatabiri kuwa huenda zingeweza kufanikiwa kuchukuwa tuzo bora.

Mahershala Ali muigizaji katika Green Book alishinda tuzo ya Muigizaji Msaidizi Bora kwa ajili ya umahiri aliyouonyesha ndani ya filamu hii. Ambapo pia alishinda tuzo za Oscar 2017 kwenye filamu ya Moonlight.

Green Book iliingia mtaani Novemba mwaka 2018, filamu iliyogharimu bajeti ya dola milioni 23 na imeingiza mauzo ya dola milioni 83.5 na mkurugenzi wake alikuwa Peter Farrelly.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC

XS
SM
MD
LG