Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 05:35

Tunisia yamwondoa afisa wa Marekani nchini kwake


Rais wa Tunisia Kais Saied akipiga kura ya maoni ya katiba mpya.
Rais wa Tunisia Kais Saied akipiga kura ya maoni ya katiba mpya.

Katika taarifa iliyotolewa na wizara hiyo ya Tunisia imesema kuwa, Waziri wa mambo ya nje wa Tunisia Othman Jerandi alimwambia kaimu balozi wa Marekani Natasha Franceschi kwamba kauli hiyo inawakilisha kuingiliwa mambo ya ndani ya kitaifa, jambo lisilokubalika.

Blinken alieleza wasiwasi kuhusu demokrasia ya Tunisia wiki hii baada ya rais Kais Saied kutangaza katiba mpya na kujipa madaraka zaidi lakini hisia pana kuhusu demokrasia ya magharibi zilinyamazishwa.

Tunisia imekumbwa na kuporomoka kwa kutisha kwa kanuni za demokrasia mwaka uliopita na kugeuza mafanikio ya watu wa Tunisia yaliyopatikana kwa bidii mwaka 2011, Blinken alisema wakati huo akimaanisha mapinduzi ya mwaka 2011 ambayo yalileta demokrasia.

Katiba mpya iliidhinishwa katika kura ya maoni iliyofanywa na rais siku ya Jumatatu mwaka mmoja baada ya Saied kutoa hoja ya kulifunga bunge lililochaguliwa na kuanza kutawala kwa amri.

XS
SM
MD
LG