Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 01:50

Tunisia kuandaa uchaguzi Oktoba 6


Rais wa Tunisia Kais Saied akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura mwaka 2023
Rais wa Tunisia Kais Saied akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura mwaka 2023

Rais wa Tunisia, anayeonekana ni mtawala wa kiimla, ametangaza kwamba uchaguzi wa urais nchini humo umepangwa kufanyika mwezi Oktoba.

Rais Kais Saied hata hivyo hajasema iwapo atagombea muhula wa pili madarakani baada ya kuiongoza nchi hiy ya Afrika kaskazini kwa muda wa miaka mitano.

Kulingana na taarifa kutoka ofisi ya rais, uchaguzi utafanyika Oktoba 6. Muhula wa kwanza wa Saied unakamilika Oktoba 23.

Uchaguzi huo utakuwa fursa ya kwanza kwa wapiga kura kutathmini utendakazi wa Saied, wakati Tunisia inakabiliwa na mgogoro wa kifedha na kuongezeka kwa utawala wa kimabavu.

Saied aliingia madarakani mwaka 2019 kwa ahadi ya kupambana na ufisadi baada ya kutokea maandamano ya kiarabu yam waka 2011 yaliyoondoa madarakani utawala wa Kidikteta.

Hata hivyo, alibadilisha baadhi ya mafanikio ya kidemokrasia yaliyokuwa yamepatikana, kuandika upya katiba ya nchi na kujitwika madaraka zaidi, kuwafunga jela wakosoaji wake wakiwemo wapinzani kutoka vyama vikubwa vya upinzani.

Forum

XS
SM
MD
LG