Mvutano ulizuka tena kati ya DRC na jirani yake Rwanda, serikali ya DRC ikiishtumu Rwanda kuunga mkono waasi wa M23, tuhuma ambazo zinakanushwa na serikali ya Rwanda.
Baada ya ziara yake nchini Afrika Kusini, Blinken anaelekea wiki hii nchini DRC, na baadaye nchini Rwanda.
Leo Jumanne, Blinken atapokelewa jioni na rais Tshisekedi ambaye “bila shaka atagusia masuala ya ushirikiano wa kimkakati kati ya DRC na Marekani,” ofisi ya rais wa DRC imesema katika taarifa.
Ofisi hiyo imeongeza kuwa “ripoti ya hivi karibuni ya wataalam wa Umoja wa mataifa kuhusu uvamizi wa wanajeshi wa Rwanda waliojificha katika kundi la M23 itajadiliwa bila shaka.”