Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:25

Trump yupo salama baada ya jaribio la mauaji


Mgombea urais wa chama cha Republican, Donald Trump, alikuwa salama baada ya kile FBI ilisema inaonekana ni jaribio la mauaji Jumapili alipokuwa akicheza gofu kwenye uwanja wake wa West Palm Beach, Florida.

Maafisa wa usalama wamesema maafisa wa idara ya ulinzi wa viongozi ya Marekani walimwona na kumfyatulia risasi mtu aliyekuwa na bunduki katika baadhi ya vichaka karibu na eneo hilo akiwa na bunduki aina ya AK-47.

Vyombo vya habari, vikiwemo The Associated Press, The New York Times na Fox News Channel, vilimtaja mshukiwa huyo kuwa ni Ryan Wesley Routh, 58, wa Hawaii, vikiwanukuu maafisa wa sheria ambao hawakutajwa majina.

Maafisa waliomtambua mshukiwa walizungumza kwa sharti la kutotajwa jina kwa sababu hawakuidhinishwa kujadili uchunguzi unaoendelea.

Reuters haikuweza kuthibitisha ripoti hizo.

Forum

XS
SM
MD
LG