Trump mara nyingi amekuwa akilalamika juu ya China kuiba kazi za Marekani. Lakini alituma ujumbe wa tweet kuwa anashirikiana na Rais wa China Xi Jinping kupunguza makali ya kuanguka kiuchumi kwa kampuni hiyo ya ZTE.
“Kazi nyingi zimetoweka China. Wizara ya Biashara imeamrishwa kurekebisha hilo!” Trump alituma ujumbe wa tweet Jumapili, siku chache baada ya kampuni ya ZTE kutangaza imesimamisha “shughuli za operesheni zake kuu.”
Marekani ilikuwa imesimamisha kuiuzia vipuli vinavyotengenezwa Marekani kampuni ya ZTE – zaidi ya asilimia 25 za vipuli hivyo vinahitajika na ZTE kutengeneza vituo vya mawasiliano ya simu, mitandao ya mkongo na simu za mkononi za kisasa.
Wizara ya Biashara ya Marekani iliikatia kampuni ya ZTE kupata vipuli vinavyotengenezwa Marekani hadi mwaka 2015, na kusababisha operesheni zake kufungwa katika kiwanda chake huko mji wa Shenzhen
Kitendo cha Marekani kuzuia kampuni ya ZTE kununua vipuli kimekuja baada ya kampuni hiyo kwa maelezo ya mtaalamu mmoja, “kukamatwa na kidhibiti” ikitumia teknolojia ya Marekani katika bidhaa zake na kuuza bidhaa hizo nchi nyingine ziliwekewa vikwazo vya biashara na Marekani, ikiwemo Iran na Korea Kaskazini.
Marekani iliitoza faini ya Dola za Marekani bilioni 1.2 kampuni ya ZTE mwaka 2017.