Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 25, 2024 Local time: 03:09

Trump aahidi kuteua mawaziri zaidi hivi karibuni


Gavana wa zamani wa Oklahoma, Mary Fallin, na gavana wa zamani wa Texas, Rick Perry, walipofika kwenye jengo la Trump Tower mjini New York, Nov. 21, 2016.
Gavana wa zamani wa Oklahoma, Mary Fallin, na gavana wa zamani wa Texas, Rick Perry, walipofika kwenye jengo la Trump Tower mjini New York, Nov. 21, 2016.

Rais mteule wa Marekani Donald trump, alisema Jumatatu kuwa atatangaza uteuzi zaidi wa mawaziri na maafisa wengine kwenye serikali yake hivi karibuni. Trump aliendelea kukutana na wanasiasa na watu ambao huenda akawateua kujiunga na baraza lake la mawaziri.

Siku ya Jumapili, Trump, akiwa katika makazi yake ya mapumziko ya kifahari yenye uwanja wa mchezo wa Golf huko Bedminster, katika jimbo la new Jersey, alikutana na washauri wake wawili wakuu walomuunga mkono wakati wa kampeni zake za kuwania urais, meya wa zamani wa new York, Rudy Guiliani na gavana wa New Jersey, Chris Christie.

Guiliani, akiwa mfano wa ukakamavu wa Marekani kupambana na ugaidi wa kislamu baada ya mashambulizi ya ugaidi ya mwaka 2001 kwenye mji wa New York na mjini Washington, hana uzoefu katika masuala ya nje lakini anataka kuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani, nafasi ya juu ya kidiplomasia katika nchi.

Wakati huo huo, Makamu rais mteule Mike Pence alikiambia kituo cha televisheni cha Fox kwamba Mitt Romney, mgombea wa zamani wa urais mwaka 2012 ambaye alikutana na Trump siku ya jumamosi, yupo kwenye orodha ya watu wanaodhaniwa kupatiwa nafasi ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani.

XS
SM
MD
LG