Vita vipya vya maneno vimezuka mjini Washington kati ya Rais Donald Trump na Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi kutokana na kuongezeka kwa uchunguzi unaofanywa na wabunge kwamba Trump alihusika katika kuficha ukweli wa mambo.
Trump anayegombania kiti cha rais Marekani mwaka 2020 alisema hatofanyakazi na wa-Demokrats juu ya masuala ya kukarabati miundo mbinu au jambo jingine lolote hadi uchunguzi unaofanywa juu yake unamalizika.
Sauti ya Amerika ilizungumza na mchambuzi wa masuala ya kisiasa Profesa Patrick Nighula wa chuo kikuu cha South Carolina na kumuuliza iwapo rais hataki kufanya kazi na wademocrats ni namna gani wataweza kufikia matakwa ya wananchi waliowapigia kura.
Ugomvi huu ulianza Jumatano wakati Rais Trump alipowasili bila kutarajiwa mbele ya waandishi wa habari walioitwa ghafa kwenye bustani ya Rose Garden. Trump aliwasili hapo baada ya kuvunja mkutano uliopangwa ndani ya ofisi yake na viongozi wa bunge wademokrats ili kujadili juu ya miradi ya kukarabati miundo mbinu ya nchi.
Trump alikua anazungumzia matamshi yaliyotolewa na spika wa baraza la wawakilishi Nancy Pelosi baada ya kukutana na wademokrats bungeni kujadili suala la uwezekano wa kumfunglia mashtaka rais.
Tangu wakati huo viongozi hao wawili kwa siku nzima wamekuwa wakirushiana maneno kwenye majukwa na matukio mbali mbali.
Trump na wademokrats wanaodhibiti baraza la wawakilishi la bunge wako katika mvutano mkali wa kupigania madaraka juu ya uwezo wa wabunge kumchunguza rais baada ya kumalizika kwa uchunguzi wa Mueller juu ya ikiwa Russia iliingilia kati uchaguzi wa marekani 2016.
Trump anasema hawezi kufanya kazi na wademnokrats katika mazingira kama haya. Hivyo anawataka kuacha kabisa uchunguzi huo wa uwongo.
Muda mfupi baadae mkuu wa wachache katika baraza la seneti Chuck Schumer alimshutumu rais kwa kupanga kwa makusudi tukio la Jumatano kama kisababu cha kukwepa majadiliano.
Wachambuzi wanasema mvutano huu kwa upande mmoja ni kichekesho lakini wakati huo huo ni tukio muhimu ambalo halifahamiki lita athiri vipi kazi za vyombo hivyo viwili vya utawala.