Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 00:16

Trump awasili Saudi Arabia kukutana na Viongozi wa Kiislam

Rais Donald Trump afanya mazungumzo mafupi na Mfalme wa Saudi Salman Bin Abdulaziz
Rais Donald Trump afanya mazungumzo mafupi na Mfalme wa Saudi Salman Bin Abdulaziz

Rais Donald Trump amewasili Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia kuanza ziara yake ya kwanza kama rais atakutana na viongozi wa Kiislam

Mfalme wa Saudi Salman Bin Abdulaziz amempokea rais na mkewe, Melania, kwenye uwanja wa ndege.

Rais Donald Trump na mkewe Melania Trump wakilakiwa na Mfalme Salman mara baada ya kuwasili Saudi Arabia
Rais Donald Trump na mkewe Melania Trump wakilakiwa na Mfalme Salman mara baada ya kuwasili Saudi Arabia

​Mfalme na familia ya Trump walitembea katika zulia jekudu wakati wakielekea kwenye ukumbi wa kifalme, katika mashukio ya ndege hapo uwanjani, ambapo walifanya mazungumzo mafupi.

Baada ya muda mfupi, Trump, akiwa na Mfalme wa Saudi waliondoka airport katika gari maalum, wakielekea mjini kupitia njia ambazo hazina msongamano wa magari.

XS
SM
MD
LG