Tajiri Donald trump, anayetazamiwa kuwa mgombea urais kupitia chama cha Republican, analalamika kuwa baadhi ya Warepublican wanajaribu hatua za mwisho mwisho kumnyima uteuzi huo katika mkutano mkuu wa uteuzi mwezi ujao.
Baadhi ya wajumbe katika mkutano mkuu utakaofanyika Cleveland, Ohio, wanasema wanataka kubadilisha sheria za chama kuruhusu wajumbe kumpigia kura mtu mwingine kuliko tajiri huyo ambaye aliwashinda wagombea wengine 16 katika miezi ya kura za awali kwenye majimbo.
Lakini wapinzani wa Trump wanasema tajiri huyo hawakilishi sera za kikonsevativu za chama hicho na kwamba matamshi yake ya kuudhi kuhusu wanawake, waislamu na Wamexico yanamfanya asiwe mtu anayebeba msimamo wa Kirepublican.
Wapinzani wa trump pia wanaonyesha matokeo ya utafiti wa kura za maoni za hivi karibuni ambazo zinaonyesha yuko nyuma waziri wa zamani wa marekani Hillary Clinton ambaye anatazamiwa kuteuliwa kama kama mgombea wa chama cha democratic.