Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:08

Trump, Kenyatta wajadili kupambana na ugaidi


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Rais wa Marekani Donald J. Trump amezungumza Jumatatu na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya huku akisisitiza kuwepo kwa ushirikiano wenye nguvu baina ya nchi hizo mbili.

Viongozi hao wamezungumzia ushirikiano wa kiuchumi na juhudi zao za pamoja katika kuushinda ugaidi na masuala mengine yanayohusu changamoto za kiusalama, wakikubaliana kuwa na ushirikiano wa karibu.

Rais Trump ameeleza kuridhishwa kwake kwa mchango muhimu wa Kenya katika kuchangia ulinzi wa majeshi ya Umoja wa Afrika huko Somalia na anatambua kujitolea kwa vikosi vya jeshi la nchi hiyo katika kupambana na al-Shabaab.

Viongozi hao wawili pia wamejadili njia za pamoja katika kuboresha biashara na uwekezaji nchini Kenya na kwa eneo lote la Afrika Mashariki.

XS
SM
MD
LG