Trump amewalaumu kwamba wameeleza vibaya maelezo yake kufuatia ghasia mbaya iliyotokea mwishoni mwa juma huko Charlottsville Virginia.
Awali siku ya Jumamosi Trump alitupa lawama kwamba ghasia hizo zinatoka “pande zote mbili”.
Baadae Jumatatu aliwashutumu wazungu wenye misimamo ya kibaguzi na Kuklux Klan kwa kuhusika kwao katika ghasia .
Ilipofika jumanne Trump alibadili msimamo kurudia wa awali kuhusu ghasia hizo zilizopelekea kifo cha Heather Heyer mwenye umri wa miaka 32 na kujeruhi wengine 19.
Mtu mmoja mwenye kuunga mkono sera za Kinazi aliendesha gari kwenye kundi la watu waliokuwa wakipinga wale wenye misimamo ya kibaguzi.