Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 27, 2024 Local time: 10:32

Trump ataka nchi nyingine kuiga sera ya 'Amerika Kwanza'


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Rais wa Marekani Donald Trump ametetea vikali sera yake ya “Amerika Kwanza” wakati akihutubia mkutano huko Davos wa viongozi wafanaybiashara Duniani na wanasiasa, akisema kuwa Marekani yenye nguvu itanufaisha dunia nzima.

Wakati wa hotuba yake ya mkutano wa Baraza la Uchumi Duniani, Trump amewaambia viongozi kwamba Marekani imeanza kuona kukua kwa uchumi wake baada ya miaka kadhaa ya kurudi nyuma, akisema sera zake ndio zilzosaidia.

Amesema kuwa kwa kupunguza kodi na kanuni, Marekani inajikomboa kibiashara na kukomboa wafanyakazi wake katika hatua ya kuwawezesha kubuni mazingira bora ya kibiashara.

Kuhusu ajenda yake ya “Marekani Kwanza” ambayo wachambuzi wanasema baadhi ya wanaharakati wanaochambua sera za kiuchumi na mambo ya nje walioko katika mkutano huo wanatilia mashaka, Trump ametaka kuwahakikishia viongozi kwamba sera zake ni nzuri kwa watu wote.

Trump amesema :“Kama rais wa Marekani, siku zote nitaitanguliza Marekani kwanza, kama inavyopaswa kufanywa na viongozi wa nchi nyingine kuzitanguliza nchi zao kwanza. Lakini Marekani kwanza haimaanishi Marekani peke yake. Wakati Marekani ikifanikiwa na ulimwengu pia utapata mafanikio.

XS
SM
MD
LG