Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 18:06

Trump apokea muhtasari wa siri juu ya Rasi ya Korea


Rais Donald Trump na mkewe Melania Trump, wakiwa na Kamanda Admirali Harry Harris, kushoto, na mkewe Bruni Bradley, wakipeperusha maua walipotembelea eneo la kumbukumbu la Pearl Harbor Memorial katika mji wa Honolulu, Hawaii, Novemba. 3, 2017.
Rais Donald Trump na mkewe Melania Trump, wakiwa na Kamanda Admirali Harry Harris, kushoto, na mkewe Bruni Bradley, wakipeperusha maua walipotembelea eneo la kumbukumbu la Pearl Harbor Memorial katika mji wa Honolulu, Hawaii, Novemba. 3, 2017.

Wakati Rasi ya Korea ikiwa katikati ya mgogoro unaoendelea hivi sasa, Rais Donald Trump amepokea muhtasari wa taarifa za siri Ijumaa kutoka kwa Kamanda wa majeshi ya Marekani katika eneo la bahari ya Pacific.

Taarifa hizo alizipokea baada ya ndege ya rais ya Air Force One kutuwa kwenye kituo cha jeshi la anga katika kisiwa cha Oahu, Pacific ambako yeye na mkewe Melania Trump walikaribishwa kwa kupewa mashada ya maua yanayojulikana kama leis, ikiwa ni utamaduni wa watu wa Hawaii.

Rais alipokea shada hilo lenye rangi ya kuvutia lililotungwa kwa maua yanayojulikana kama maile na ilima, ambao hutolewa katika utamaduni wa nchi hiyo kwa mfalme wa visiwa hivyo. Shada alilopokea mkewe Trump lilikuwa limetungwa kwa maua ya yasmini na mawardi.

Trump atembelea kikosi cha wanamaji

Rais Trump baadae alielekea moja kwa moja kwenye kituo cha askari wa jeshi la majini ambapo kikosi cha Pacific, kikubwa katika vikosi vilivyounganishwa pamoja, chenye makao yake makuu Hawaii.

“Mna watu wakakamavu wengi na watu wenye vipaji na hili linatufurahisha,” Trump alimwambia Admirali wa Jeshi la Majini la Marekani, Harry Harris, ambaye ni kamanda wa Kikosi cha Pacific.

“Tunayoheshima kubwa kuja kwenu katika kisiwa hiki,” Harris alijibu kabla ya wote wawili kupeana mikono mbele ya kamera na waandishi wa habari kusindikizwa nje ya ukumbi.

Mkutano wa Asia Mashariki

Wakati Trump akiwa safarini ndani ya ndege ya Air Force One, amesema anataka kukaa kwa siku moja zaidi Hawaii baada ya kile alichokiita ni “ziara mhimu sana,” lakini alibadili mawazo juu ya kuendelea kukaa ili apate muda zaidi wa kukaa Ufilipino ambako anahudhuria Mkutano wa marais wa nchi za Asia Mashariki, pamoja na mkutano wa viongozi wa umoja wa nchi za kusinimashariki mwa Asia(ASEAN).

“Kama raia, sisi tutawawakilisheni vizuri. Sawa? Kama waandishi, mimi sijui,” Trump, aliyezungumza kwa ufupi sana na waandishi kwenye ndege, alisema hayo katika safari ya masaa kumi kutoka kituo cha kijeshi cha Joint Base Andrews huko Maryland, Marekani hadi kuwasili Hawaii huko katikati ya Bahari ya Pacific.

Nchi atazotembelea Trump

Kabla ya Trump kufika Ufilipino, ziara yake ya siku 13 itamfikisha hadi Japan, Korea Kusini, China na Vietnam, safari ndefu kuliko zote akiwa rais.

Wakati wa mikutano yake na viongozi wengine, rais atawaambia viongozi hao kuwa dunia “haina muda tena wakusubiri” katika kuzuia sila za nyuklia na makombora ya balistiki yanayotengenezwa na Korea Kaskazini, ambapo viongozi wa serikali ya Marekani wanaona ndio tishio kubwa kabisa.

“Mazungumzo yatajiri katika mtizamo wa jambo gani jingine lifanyike kulitatua tatizo hili, bila ya kuingia vitani, tukitambua kuwa sote tunakabiliwa na ufinyu wa wakati kukabiliana na hili,” kwa mujibu wa Mshauri wa Usalama Taifa H.R McMaster. “Marekani, Korea Kusini, Japan, China hawana muda tena kusubiri juu ya suala hili.”

XS
SM
MD
LG