Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 20:03

Trump apiga marufuku wasafiri kutoka Brazil kuingia Marekani


Rais wa Brazil Jair Bolsonaro na Rais wa Marekani Donald Trump.
Rais wa Brazil Jair Bolsonaro na Rais wa Marekani Donald Trump.

Utawala wa Rais Donald Trump, Jumapili ulitangaza marufuku ya wasafiri ambao si raia wa Marekani, kuingia nchini kutoka Brazil katika kile ulichokiita "juhudi za kukabiliana na ongezeko la maambukizi ya Corona."

Kupitia amri iliyotangazwa na White House, wasafiri waliokuwa kwenye ardhi ya Brazil kwa siku 14 kabla ya siku yao ya kusafiri, hawatarushusiwa kuingia Marekani.

Hata hivyo, raia wa Marekani pamoja na jamaa zao, au watu walio na vyeti maalum vinavyowaruhusu kuishi au kufanya kazi Marekani, maarufu Green Card, wako huru kuingia.

Aidha marubani na wafanyakazi wengine wa ndege hawatazuiliwa kuingia Marekani, kwa mujibbu wa taarifa ya ikulu.

Trump pia alitangaza kuongezwa kwa muda wa zuio la wasafiri kutoka nchi za ulaya, China, Uingereza, Ireland na viswa vya Macau.

Kwa mujibu wa takwimu za chuo cha Johns Hopkins, Brazil kimekuwa kitovu kipya cha maambukizi ya Corona huku ikiwa tu inashindwa na Marekani kwa idadi ya watu waliopata ugonjwa huo.

Takriban watu 22,000 wamekufa nchini Brazil Kutokana na ugonjwa huo. Marekani bado inaongoza kwa idadi ya vifo nay a maambukizi, ikirekodi vifo vya watu 97,000 na maambukizi takriban milioni 1.6 , kufikia Jumapili.

Mwezi Machi mwaka huu, Rais Trump alitanzaza zuio kwa raia wa nchi za Ulaya kuingia nchini Marekani ili kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona.

Katika hotuba yake kutoka Ikulu mjini Washington DC, Trump wakatiu huo alisema safari zote za kutoka Ulaya zingezuiwa kwa siku 30. Baadaye, White House ilifafanua kwamba amri hiyop haikuwahusu raia wa Marekani na familia zao au watu ambao wana vyeti rasmi kuwaruhusu kuishi Marekani.

XS
SM
MD
LG