Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 05:46

Trump aongoza kwa kura katika mkutano wa CPAC


Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alipohudhuria Kongamano la Kihafidhina la Kisiasa (CPAC) katika Kituo cha Mikutano cha Kitaifa cha Gaylord huko National Harbor, Maryland, Marekani, Machi 4, 2023.REUTERS
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alipohudhuria Kongamano la Kihafidhina la Kisiasa (CPAC) katika Kituo cha Mikutano cha Kitaifa cha Gaylord huko National Harbor, Maryland, Marekani, Machi 4, 2023.REUTERS

Matukio mawili ya kushindana yameonyesha mgawanyiko wa waconservative wa Marekani kabla ya uchaguzi mkuu wa rais mwaka ujao.

Wakati Donald Trump na mpinzani pekee aliyetangaza atawania urais balozi wake wa zamani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley, walipanda jukwaani katika mkutano wa Kisiasa wa Waconservative karibu na Washington, wengine walihudhuria mkutano wa faragha huko Florida ulioandaliwa na Club for Growth.

Rais wa zamani Donald Trump alirejea kwenye uwanja wa siasa aliouzoea na wa kirafiki kwake Jumamosi usiku katika ukumbi wa mkutano wa kila mwaka wa CPAC, ambapo waliohudhuria walimuunga mkono kwa asilimia 62 katika kura ya mchujo wa awali ya kutafuta mgombea wa Chama cha Republican mwaka ujao.

" Mwaka 2016 nilitangaza: Mimi ni sauti yenu. Leo, naongeza: Mimi ni shujaa wenu. Mimi ni haki yenu. Na kwa wale walio dhulumiwa na kufanyiwa hiyana, mimi ni mlipizaji wenu. Mimi ndiye mlipaji kisasi wenu" alisema Trump.

Mpinzani pekee mkubwa, wa Trump aliyetangaza kuwania urais pia alizungumza katika huko mkutano wa CPAC alikuwa balozi wake wa zamani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley.

"Niko hapa kuomba kura zenu. Lakini nataka jambo jingine zaidi nataka tuihamasishe nchi yetu tena" alisema Nikki Haley.

Mgombea mwingine mtarajiwa wa chama cha Republican ambaye hajajitangaza pia alihutubia CPAC alikuwa ni Mike Pompeo, mmoja wa mawaziri wa serikali ya Trump. Alichukua kile kilichoonekana kama kumkosoa kwa staha bosi wake wa zamani.

"Tunahitaji chama, chama cha Conservative, ambacho tunaweza kujivunia na kukiita cha nyumbani kwa mara nyingine tena, chenye msingi wa mawazo ya waasisi wetu, kikiongozwa na watu kweli, chenye uwezo na kujitolea kwa sababu za msingi ambazo zimetuleta sisi wote hapa hivi leo" Alisema Mike Pompeo, Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani.

Haley pia alizungumza kwenye tukio lililofanyika Florida, ambayo liliandaliwa na kundi la waconservative, linalolenga katika kodi na uchumi la Club for Growth. Tukio hilo lilifanyika kwa faragha.

Hotuba iliyotarajiwa kwa hamu katika mkutano huo wa Club for Growth ambao Trump hakualikwa, ilitoka kwa Gavana wa Florida Ron DeSantis. Anayeonekana kuwa tishio kubwa zaidi kwa azma ya Trump ya kushinda tena uteuzi wa chama chake kuwa rais.

Katika kura ya Jumamosi ya taasisi ya CPAC, DeSantis alipata asilimia 20 ya kura, ikiashiria kuwa ana kazi kubwa ya kumng'oa Trump, haswa miongoni mwa wafuasi waaminifu zaidi wa rais huyo wa zamani.

XS
SM
MD
LG