Rais wa Marekani Donald Trump alisema ataiangalia tena kesi ya mwanajeshi mkongwe katika kikosi maalumu aliyeshutumiwa kumuuwa mwaka 2010 mshukiwa Taliban mtengenezaji bomu nchini Afghanistan.
Kiongozi wa Marekani alisema “kufuatia ombi la wengi, atapima mashtaka ya mauaji dhidi ya Meja Matthew Golsteyn, mwanajeshi wa zamani katika kikosi cha Green Beret. Kwa maneno ya Trump, Goldteyn “ataweza kukabiliwa na adhabu ya kifo kutoka katika serikali yetu baada ya mwanajeshi huyo kukubali kumuuwa gaidi mtengenezaji bomu akiwa nje ya nchi”.
Trump alimuita Golsteyn, “shujaa wa jeshi la Marekani”. Jeshi limekuwa likichunguza mazingira ya kifo cha mshukiwa mtengenezaji bomu kwa miaka kadhaa, na kuacha uchunguzi wake mwaka 2014. Baada ya hapo ilianza tena uchunguzi mwaka 2016 baada ya Golsteyn aliposema katika mahojiano na kituo cha TV cha FOX NEWS nchini Marekani kwamba alimuuwa mtengenezaji mabomu ambaye alikuwa amekamatwa katika operesheni ya mapambano huko Marjah nchini Afghanistan, kwa khofu kwamba kama atamuachia atawalenga wa-Afghanistan wanaosaidia vikosi vya Marekani.
Mshukiwa huyo mtengenezaji mabomu wa Taliban alishutumiwa kuhusika kwa vifo vya Marine wawili wa Marekani