Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 14, 2024 Local time: 09:33

Trump amemteua Elise Stefanik kuwa balozi wa Marekani katika UN


Rais mteule wa Marekani, Donald Trump akiwa na Elise Stefanik, mwakilishi wa New York kwa chama cha Republican. Jan. 19, 2024.
Rais mteule wa Marekani, Donald Trump akiwa na Elise Stefanik, mwakilishi wa New York kwa chama cha Republican. Jan. 19, 2024.

Trump alisema Elise ni mpiganaji imara, mwenye nguvu, na mwerevu  anayeliweka taifa kwanza.

Donald Trump amemchagua mwakilishi wa Republican Elise Stefanik kuwa balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, rais mteule amesema katika taarifa yake iliyosambazwa na shirika la habari la Reuters leo Jumatatu.

Kwa heshima kubwa ninamteua, mwenyekiti Elise Stefanik kuhudumu katika baraza langu la mawaziri kama balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa. Elise ni mpiganaji imara, mwenye nguvu, na mwerevu anayeliweka taifa kwanza, Trump alisema.

Stefanik, mwakilishi wa New York na mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi la Republican, amekuwa mshirika mkubwa wa Trump. Stefanik hakupatikana kwa haraka ili kutoa maoni yake.

Trump alisema Jumamosi kuwa mgombea urais wa zamani wa chama cha Republican Nikki Haley na waziri wa zamani wa mambo ya nje Mike Pompeo, hawataombwa kujiunga katika utawala wake.

Forum

XS
SM
MD
LG