Trump amesema Ijumaa kuwa William Barr, ambaye alikuwa mwanasheria mkuu wakati wa utawala wa hayati Rais wa zamani George H.W. Bush ni chaguo lake, akimuelezea kama mtu mwema, na mtu mahiri.
Rais amewaambia waandishi wa habari wakiwa White House kwamba Barr, ambaye ni Mrepublikan, M-Conservative mwenye umri wa miaka 68 na ni wakili wa kampuni, “ alikuwa chaguo langu tangu siku ya kwanza. Anaheshimiwa na Warepublikan na kuheshimiwa na Wademokrat.”
Barr atamrithi kaimu Mwanasheria Mkuu Matthew Whitaker, ambaye aliteuliwa na rais kuongoza Wizara ya Sheria mwezi uliopita baada ya Trump kumfukuza kazi Jeff Sessions, ambaye ni Seneta wa Marekani wa zamani na mmoja wa wale walio muunga mkono Trump hapo awali katika uchaguzi mkuu 2016.