Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 07:43

Trump akata rufaa dhidi ya uamuzi wa jimbo la Maine


Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, Jumanne amekata rufaa juu ya uamuzi wa katibu wa chama cha Demokrat, katika jimbo la Maine, wa kumuondoa katika karatasi ya kura kutokana na ushiriki wake kwenye  tukio la Januari 6, 2021 katika bunge la Marekani.

Alitarajiwa pia kuiomba mahakama ya juu ya Marekani, iamue kwa upande wake na kumrejesha katika karatasi ya kura katika shauri linalofanana katika jimbo la Colorado.

Mgombea huyo wa chama cha Republikan amekata rufaa dhidi ya uamuzi wa Shenna Bellows, ambaye amekuwa katibu wa kwanza wa jimbo kumzuia mtu kugombea urais chini ya sheria nadra ya kifungu cha tatu katika marekebisho ya ibara ya 14 ya katiba.

Kifungu hicho kinawapiga marufuku wale ambao wanajihusisha na uasi wakiwa madarakani.

Rufaa yake sasa inapelekwa katika mahakama ya juu ya jimbo la Maine.

Forum

XS
SM
MD
LG