Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 15:43

Mtalii auawa na Tembo Kenya


Tembo akinywa maui wakati anavuka Mto Mara, Maasai Mara, Kenya, July 6, 2015.
Tembo akinywa maui wakati anavuka Mto Mara, Maasai Mara, Kenya, July 6, 2015.

Polisi nchini Kenya anasema mtalii mmoja kutoka Italia ameuliwa na tembo katika jimbo la Pwani baada ya kumsogelea kupiga picha.

Mkuu wa polisi wa Malindi Muchangi Mutava amewaambia waandishi kuwa mtu huyo mwenye umri wa miaka 66 alimwona tembo akinywa maji kwenye dimbwi Jumapili karibu na kambi ya Swara katika mbuga Kulalu na kumsogolea kupata picha nzuri zaidi.

Kitendo hicho bila shaka kilimwuudhi tembo huyo ndipo alipomshambulia Mtaliani huyo na kumjeruhi vibaya na kufariki baadaye katika kambi hiyo.

Mutava alisema mtalii huyo alikuwa na mkewe katika ziara ya kitalii ambayo kulingana na visa zao ilikuwa wawepo nchini Kenya mpaka mwezi ujao.

Mbuga ya Kulalu inavutia watalii wengi pwani ya Kenya kwa sababu ina aina mbali mbali ya wanyama pori.

XS
SM
MD
LG