Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 07:51

Timu ya US Monastir yakata tiketi ya kwanza kuingia robo fainali ya BAL


Wachezaji wa US Monastir Charles Onana (Kushoto) na Radhouane Slimane
wakisherehekea ushindi wao wa jumla ya pointi 74-62 dhidi ya Dakar University Club-DUC Jumamosi katika Uwanja wa Dakar Arena.(Picha na BAL).
Wachezaji wa US Monastir Charles Onana (Kushoto) na Radhouane Slimane wakisherehekea ushindi wao wa jumla ya pointi 74-62 dhidi ya Dakar University Club-DUC Jumamosi katika Uwanja wa Dakar Arena.(Picha na BAL).

Timu ya US Monastir ya Tunisia ilikuwa ya kwanza kukata tiketi ya kuingia robo fainali ya michuano ya BAL baada ya kuishinda timu ya Dakar University Club-DUC  kwa jumla ya pointi 74-62 siku ya Jumamosi.

Kocha Mkuu wa Monastir, Modrag Perisic alihusisha ushindi wa timu yake dhidi ya DUC na juhudi kubwa za timu, lakini pia juhudi za wachezaji wake hatari Ater Majok na Firas Lahyani walivyoshiriki mchezo huo akisema haiwezi kupuuzwa.

Wawili hao walionyesha ukali wa hali ya juu dhidi ya DUC siku ya Jumamosi kusaidia timu ya Monastir ya Tunisia kufanikiwa kuingia kwenye hatua ya robo fainali kwa kucheza mechi nne bila kushindwa katika kanda ya Sahara.

Majok aliifikisha timu hiyo yenye maskani yake Monastir kwa pointi 20 na rebounds 13 ikiwa ni mechi yake ya kufunga pointi za tarakimu mbili katika maeneo mawili katika mechi kadhaa alizocheza na goli lao kwa kuzuia mara nne huku Lahyani akiwa ameingiza mpira nyavuni mara 8 kati ya 10 alizorusha mpira golini na kumaliza akiwa na pointi 19 na rebound nane.

Ingawa mashabiki wa nyumbani wa timu ya DUC walionyesha ari ya kuwashangilia wachezaji wao dhidi ya mpinzani mkali, lakini hawakuweza kufua dafu kwa timu ya US Monastir ambayo ilitawala katika kila eneo la mchezo huo.

XS
SM
MD
LG